P-FUNK AANGUKA CHOONI NA KUPATA JERAHA KARIBU NA JICHO
Paul Matthysse ‘P-Funk’ akionesha jeraha alilolipata kichwani baada ya kuanguka chooni.
LEGEND wa
kuzalisha mapigo ya muziki Bongo, Paul Matthysse ‘P-Funk’, amepata ajali
ya kushangaza chooni, nyumbani kwake, Mwenge Kijijini, Dar es Salaam.P
alidamka alfajiri kwenda msalani kujisevu mambo ya short-call, akiwa
huko alishikwa na kizunguzungu cha ghafla kisha akaanguka kama mzigo.Ajali
hiyo, ilimkuta P alfajiri ya Ijumaa iliyopita na kuhusu hilo, mwenyewe
alifunguka: “Nilishangaa sana, unajua siku hiyo sikuwa nimekunywa pombe
kusema labda nilikuwa nimelewa, nilishangaa tu napatwa na kizunguzungu
kisha nikaanguka.