SIKU chache baada ya ndoa ya mwigizaji, Ndubagwe Mithayo ‘Thea’
kuvunjika, mwigizaji Deogratius Shija ‘Shija’ ameibuka na kueleza
maumivu anayoyapata juu ya tukio hilo.
Akizungumza na Amani hivi karibuni, Shija alisema taarifa za
kuvunjika kwa ndoa ya Thea na Mike Sangu zilimuuma na kuwataka vijana
wengi kuwa makini kabla ya kuoa na haswa kumshirikisha Mungu kila siku
kwenye maombi ili ndoa zao zidumu.
“Ndoa siyo maigizo. Ndoa ni mkataba mkubwa sana ambao wanaingia
wanadamu hivyo inapovunjika huwa haileti picha nzuri kwa Mungu, binafsi
inaniuma sana,” alisema Shija.