VIDEO Queen wa Bongo, Agnes Gerald Waya ‘Masogange’ ambaye alipata
soo la kukamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine Julai 5, mwaka
huu nchini Afrika Kusini amejaa tele jijini Dar es Salaam, Ijumaa
limethibitisha.
Masogange ambaye siku ya tukio alikuwa na nduguye, Melisa Edward
baada ya kunaswa na madawa hayo kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa
Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo
alihukumiwa kwenda jela miezi 32 au kulipa faini ya shilinghi milioni
4.8 ambapo aliweza kulipa na kuwa huru.
Tangu aachiwe huru, Septemba mwaka huu, msanii huyo akawa hajulikani
alipo huku baadhi ya ‘posti’ zake kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram
zikionesha yupo Tanzania au Afrika Kusini.
Jumatatu iliyopita, mida ya saa kumi jioni, paparazi wetu alipigiwa
simu na msomaji wa gazeti hili (jina tunalo) akisema amemwona Masogange
akiingia kwenye duka la nguo lililopo Sinza Kamanyola, Dar akiwa peke
yake.
Paparazi wetu alijipanga kwa kamera na kutia timu kwenye duka hilo
ambapo hata hivyo muuzaji alisema aliondoka baada ya kufanya manunuzi ya
kawaida.
Jumatano, Masogange alitumbukiza picha kwenye mtandao wake akiwa ndani ya duka hilo na modo maarufu nchini, Jacqueline Patrick.
Jack
alipigiwa simu ambapo alikiri kuwa na Masogange siku ya Jumanne kwenye
duka hilo. Akasema: “Mimi nilimkuta pale, tukapiga picha tukaachana,
basi.”
Kwa kutumia namba yake ya simu ya mkononi, Masogange alipatikana na
kukiri yupo Dar lakini akasema hakutaka kuweka wazi kwa sababu
anawaogopa sana mapaparazi.