Wiki iliyopita akizungumza na
Menejimenti na watumishi wa Kampuni ya Uwakala wa Uendeshaji wa Kia
(KADCO), Dk Mwakyembe alisema ana taarifa za kutosha kuhusu baadhi ya
wafanyakazi wa kampuni hiyo, hasa Kitengo cha Usalama na Uhamiaji
wanaohujumu sifa za kiwanja hicho.
Alidai kuwa wafanyakazi hao wamekuwa
wakishiriki kutoa hati feki za kusafiria, kuvusha dawa za kulevya na
nyara za Serikali, jambo ambalo alionya kuwa hatalivumilia kwa kuwa
linaitia doa nchi kimataifa. Siku chache baada ya onyo hilo, wanawake
hao wawili, mmoja Mnigeria na mwingine Mliberia walikamatwa kwa nyakati
tofauti wakiwa na dawa hizo wakiwa njiani kwenda nje.
Kukamatwa kwa wanawake hao
kumethibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz
alipopigiwa simu na gazeti hili kuthibitisha tukio hilo.
Vyanzo vya habari vilisema wa kwanza
kukamatwa alikuwa raia wa Liberia, aliyekuwa na dawa za kulevya zenye
uzito wa kilo tano akiwa tayari kupanda ndege ya Shirika la Ndege la
Ethiopia kwenda Addis Ababa nchini Ethiopia saa 9 usiku.
Kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari,
mwanamke huyo raia wa Liberia alionekana hajiamini kupita kiasi na
alipokaguliwa, alikuwa na mzigo huo uliokuwa umefichwa kwa ustadi katika
mabegi yake kwa kushoneshwa kwa ndani.
Mwanamke mwingine raia wa Nigeria
alikamatwa na kilo 10 za dawa hizo saa 11 alfajiri jana akitaka kusafiri
na ndege ya Shirika la Ndege la Precision kwenda Nairobi nchini Kenya.
Habari zilisema kuwa raia huyo wa
Nigeria, alikuwa na mabegi kama ya raia huyo wa Liberia, hali
iliyosababisha atiliwe shaka kuwa huenda anafahamiana na mwenzake ingawa
walikuwa wapande ndege tofauti. Kamanda Boaz alisema kwa sasa wanawake
hao wako chini ya ulinzi wa Polisi kwa mahojiano na atakuwa tayari
kutaja majina ya watuhumiwa leo.
“Siko ofisini lakini tukio hilo lipo na
majina ya watuhumiwa nitayataja kesho (leo) kwa kuwa kila kitu kipo
ofisini… kuwa na subira,’’ alisema.
Inadaiwa baada ya Serikali kuimarisha
ulinzi na kuwabana wasafirishaji dawa za kulevya katika Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam, wafanyabiashara
hao walianza kutumia KIA kusafirishia dawa hizo haramu.
Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa KIA,
Bakari Murusuri alipokuwa akizungumza katika kikao cha Dk Mwakyembe,
alisema kati ya Machi hadi Oktoba, mwaka huu, watu watano wamekamatwa
wakisafirisha dawa za kulenya aina tofauti, zenye thamani ya mamilioni
ya fedha.