Search in This Blog

AMA KWELI WOLPER NI MAJANGA


Jacqueline Wolper Massawe.
Stori:  Gladness Mallya
SEXY lady katika tasnia ya filamu za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amepata majanga baada ya gari lake kugonga gari lingine na vitu kibao kwenye siku ya ‘bethidei’ yake.

Pichani (chini kushoto) ni gari aina ya Toyota Prado lililogonga gari lingine kulia pamoja na matenki ya maji na mabomba.
Tukio hilo lilijiri Ijumaa iliyopita nyumbani kwake Mwananyamala, Dar  akiwa anasogeza lile gari lake jipya aina ya Toyota Prado ili lioshwe ambapo aliponea chupuchupu kuuvaa ukuta.
Habari zilieleza kuwa Wolper, badala ya kukanyaga breki alijikuta akikanyaga mafuta na kusababisha abomoe matenki ya maji na kupasua mabomba yote pia kugonga gari lingine lakini hakuumia ila presha ilishuka kidogo.
“Kuzaliwa ni siku moja na kufa ni siku moja ndiyo maana kila siku nasisitiza upendo na tuache chuki zisizokuwa na sababu.
“Leo (Ijumaa) nilikuwa nauvaa ukuta ikiwa ndiyo kwanza naanza maandalizi ya kusherehekea bethidei yangu, nimebomoa matenki na nimepasua mabomba lakini yote namshukuru Mungu kwa kuwa sijaumia, asante Mungu wa wote kimbilio la wote na wewe ndiyo kimbilio langu, niombeeni jamani,” aliandika Wolper katika akaunti yake ya Instagram.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger