Search in This Blog

ARSENAL YASHINDWA KUTAMBA NYUMBANI DHIDI YA EVERTON, YATOKA SARE, ANGALIA VIDEO YA MECHI HIYO HAPA


Mesut Ozil akiifungia Arsenal bao la kuongoza katika dakika ya 80 ya mchezo.
Ozil akishangilia na wachezaji wenzake baada ya kufunga bao.
Gerard Deulofeu wa Everton (kushoto) akishangilia bao la kusawazisha dakika ya 81 ya mchezo.
Beki wa Arsenal Laurent Koscielny (kushoto) akijaribu kumzuia Steven Pienaar wa Everton wakati wa mchezo huo.
Timu ya Arsenal imeshikwa baada ya kutoka sare ya 1-1 na Everton katika mechi ya Ligi Kuu England iliyopigwa Uwanja wa Emirates jijini London, Uingereza hivi punde.
Bao la kuongoza la Arsenal limewekwa kimiani na Mesut Ozil dakika ya 80 kabla ya Gerard Deulofeu kusawazisha bao hilo dakika ya 84 na kufanya matokeo kuwa 1-1.
Mpaka mwisho wa mchezo Arsenal 1 na Everton 1. Kwa matokeo hayo bado Arsenal wanaongoza ligi hiyo wakiwa na pointi 35 wakati Everton wapo nafasi ya tano wakiwa na pointi 28.

VIDEO:

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger