Search in This Blog

BREAKING NEWS: NELSON MANDELA AAGA DUNIA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 95

Nelson Mandela, rais wa kwanza mzalendo wa Afrika Kusini afariki dunia, Tanzania yatangaza siku tatu za maombolezo

posted 3 hours ago by admin
Rais wa kwanza mzalendo wa taifa la Afrika Kusini amefariki dunia nyumbani kwake Pretoria akiwa na umri wa miaka 95 kutokana na matatizo ya mapafu.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ametangaza kwa majonzi kifo cha Mandela usiku wa manane na amesema kuwa amefariki majira ya saa mbili na nusu kwa saa za Afrika Kusini. Ametangaza siku za maombolezo na bendela zitapeperushwa nusu mlingoti.
Mandela aliwezesha kukomeshwa kwa ubaguzi wa rangi nchini Afrika kusini, na harakati zake zilipelekea kufungwa jela miaka 27.
Tanzania imetangaza siku tatu za majonzi ili kumkumbuka Nelson Mandela mbaye alifika Tanzania baada ya kutoka gerezani.
Tanzania ilikuwa karibu sana na harakati za Nelson Mandela kupitia chama cha ANC na TANU iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mwalimu Julius Nyerere.
Marais na viongozi mbalimbali duniani wametuma salam za rambirambi na wengine wakitumia akaunti ya twitter kuonesha hisia zao juu ya kifo cha Mandela.
Rais wa Marekani Barack Obama amempigia simu rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma na kufikisha salam zake za rambirambi.
Mandela alizaliwa July, 18 mwaka 1918.
Apumzike kwa amani. Amina.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger