Search in This Blog

DESEMBA 15 NDIYO SIKU ATAKAYOZIKWA MANDELA HUKO QUNU, AFRIKA KUSINI


 Nelson Mandela enzi za uhai.
Rais Jacob Zuma ametangaza kuwa mazishi ya Nelson Mandela yatafanyika siku ya Jumapili, Desemba 15 mwaka huu kijijini kwake Qunu, katika jimbo la Eastern Cape, Afrika Kusini.
Rais Zuma pia ametangaza siku 5 za maombolezo kitaifa na bendera zitapeperushwa nusu mlingoti katika muda wote huo. Na ameitangaza siku ya Jumapili ya Desemba 8, 2013 kuwa siku maalumu ya kitaifa ya maombolezo na kumkumbuka Madiba nchi nzima.
Tayari msisimko wa mazishi hayo yanayotarajiwa kuwa ya kihistoria umekamata dunia nzima, ambapo tayari Rais Obama wa Marekani, mstaafu Bill Clinton na Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ni baadhi tu ya viongozi ambao wamethibitisha kushiriki.
Sala ya mazishi imepangwa kufanyika katika Uwanja wa Taifa wa FNB Desemba 10, 2013 jijini Johanesburg.
Mwili wake utawekwa jengo la serikali liitwalo Union Buildings kuanzia Desemba 11 hadi 13, kwa kupewa heshima za mwisho, kabla ya kupelekwa kijijini Qunu kwa mazishi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger