Search in This Blog

DKT. SLAA!!: MGOGORO ULIOPO NDANI YA CHAMA NI KAZI YA MAKACHERO

*Aunguruma Kahama, kuwasili Kigoma leo
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Willibrod Slaa amesema mgogoro uliopo ndani ya chama ni kazi ya makachezo. Alitoa kauli hiyo jana jioni alipokuwa akihutubia mamia ya wananchi wa Mji wa Kahama mara baada ya kuwasili akitokea jijini Dar es Salaam akiwa njia kuelekea mkoani Kigoma kwa ziara ya wiki moja.

Dk. Slaa ambaye alifika saa 12 jioni alitumia muda dakika zisizozidi 20 kuhutubia ambapo alisema chama hicho kina taarifa za ushiriki wa makachero, lengo likiwa kukidhoofisha na hatimaye kukisambaratisha chama hicho.

“Tunazo tayari taarifa kuwa makachero ndio wapo nyuma ya mgogoro ndani ya chama, wameingia kwa nia ya kutuvuruga, lakini tupo imara.

“Nawasihi Watanzania waache kushabikia vitu visivyo vya msingi, badala watumie muda wao kufikiri na kufanya mambo ya msingi kwa Taifa.

“Yote yanayotokea katika chama chetu kwa sasa yanatuandaa na kutukomaza kwa ajira ya kuchukua madaraka ya nchi mwaka 2015,” alisema.

Alisema kuwa, wanachama wote wa Chadema wanapaswa kujua hakuna aliye juu ya Katiba ya chama hicho, kwa hiyo Katiba italindwa na kusimamiwa bila woga kwa maslahi mapana ya chama.

Leo asubuhi anatarajiwa kuondoka na msafara wake kuelekea mkoani Kigoma, ambako kituo chake cha kwanza kitakuwa eneo la Kakonko na baadae ataelekea Muhambwe.

Katika ziara hiyo ya kukagua uhai wa chama atatembelea mikoa ya Shinyanga, Kigoma, Tabora na Singida.

-MTANZANIA
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger