TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
UTANGULIZI
UTANGULIZI
Ndugu wanahabari, mbele yenu ni muunganiko
wa wawakilishi wa matawi 189 ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) mkoa wa Mwanza. Umoja huu wa matawi unawajumuisha wajumbe
kutoka majimbo yote ya mkoa wa mwanza.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30 Nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hivyo katika kikao chetu tulichoketi tarehe 30 Nov 2013 kuanzia saa nne asubuhi mpaka saa tisa kasorobo, pamoja na mambo mengine tumeazimia kuanzisha umoja huu wa wanachama.
Hii ni kutokana na ukweli kwamba viongozi
wetu wanaotuwakilisha kwenye vikao vya maamuzi kama vile wilaya, mkoa
na taifa wamekuwa waoga na wameshindwa kuwakilisha mawazo yetu
tuliyowatuma badala yake wengi wao wamekubali kuwa vibaraka wa kile
kinachoitwa CHADEMA KASKAZ
Kutokana na ukweli kwamba msingi wa chama
chetu na chama kingine chochote kile cha siasa, uimara na uhai wake
unatokana na uwepo wa misingi na matawi ya chama, hivyo sisi wanachama
wa matawi haya 189 tumeamua kuunganisha nguvu zetu kutetea chama chetu
na kuhakikisha haki, heshima, katiba na maadili ya chama vinafuatwa bila
ya kuogopana wala kuoneana haya.
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Umoja huu umeonelea ni vema kuutaarifu umma wa watanzania na wapenzi na wanachama wa chadema mambo kadhaa yafuatayo
Kwamba:-
Chadema ni chama cha siasa kinachopaswa
kuendeshwa kwa misingi ya kufuata taratibu, kanuni na katiba yake na si
vinginevyo. Lakini badala yake kwasasa kumeibuka ombwe kubwa kwa
viongozi wetu wa juu kujitwalia mamlaka ya chama kinyume na matakwa ya
katiba ya chama chetu hususan katika kutoa haki sawa kwa viongozi na
wanachama wa chama chetu. Kumekuwepo na upendeleo wa hali ya juu sana
kwa wale wanao amini kuwa ndani ya chama hawawaungi mkono hivyo
kupelekea kuwaadhibu kama ndio kinga yao ya kuendelea kuongoza bila
kuhojiwa au kukosolewa.
Sababu zilizotolewa na kamati kuu hazikubaliki
Maamuzi ya kamati kuu ya tarehe 20-21
/11/2013 ya kuwavua uongozi Mh: Zitto Zuberi Kabwe, Dr. Kitila Mkumbo na
Ndg Samson Mwigamba, kumeonyesha dhahiri si woga tu wa Demokrasia bali
ni unafki na Uzandiki wa hali ya juu sana kwa viongozi wetu kuikwepa
Demokrasia kwa kisingizio cha kusaliti na uhaini ndani ya chama.
Katiba yetu imeweka wazi Ibara ya 6 Kifungu
cha 3 kipengele cha 6. (a – f) Mamlaka za nidhamu na uwajibishaji ndani
ya chama. Kulikuwa na haraka gani ya kufanya maamuzi bila kufuata
taratibu hizi kwa viongozi hawa, tuonavyo sisi baadhi ya wanachama huo
ni umangi meza na udhalilishaji wa kibaguzi ndani ya chama kwa viongozi
wetu waliotumia nguvu zao na akili nyingi sana kukijenga chama.
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
Sababu kubwa ya kuandamwa kwa viongozi hawa ni
1. Kutaka kujua mapato na matumizi ya fedha za chama zinazotokana na Ruzuku ya fedha za serikali.
2. Michango ya wanachama na wapenzi kwenye mikutano ya wazi.
3. Harambee za M4C Mwanza, Arusha na Dar es saalam.
4. Kutaka kujua taratibu za manunuzi ya rasilimali ya chama namna walivyopatikana wadhabuni wa kusambaza bendera na kadi za chama, magari na pikipiki ambapo ununuzi wake ni wa mashaka makubwa.
5. Kutaka kuona usawa wa kimadaraka kwa viongozi wote bila ubaguzi wa aina yoyote kuanzia ngazi ya chini mpaka Taifa kinyume na ilivyo sasa hasa makao makuu ya chama ambapo ukanda na ubaguzi wa hali ya juu umetawala.
Kushamiri kwa migogoro

Mwenyekiti na katibu mkuu wameshindwa
kutatua migogoro ya viongozi na wanachama kutoka mikoani kwa njia sahihi
za vikao na kwa wakati hivyo kutoa mwanya kwa viongozi na wanachama
kutumia njia ya mitandao ya kijamii tukiongozwa na katibu mkuu mwenyewe,
kujitokeza mara kwa mara kwenye mitandao hiyo hiyo kwa madai ya kutolea
ufafanuzi ya mambo mbalimbali ya husuyo maswala ya chama ilihali akijua
kufanya hivyo ni usaliti mkubwa kwa chama chake, njia hiyo ya nje ya
vikao ilipelekea migogoro mikubwa sana hususan mkoa wetu wa Mwanza na
kupelekea kupoteza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kutokana na kufukuzwa
kwa baadhi ya madiwani, kuvunjwa uongozi wa mkoa na wabunge kuwa juu ya
chama na kutumia nafasi zao kuopanga safu za uongozi wanao uwona
watawatumikia wao na si chama, hivyo kusababisha mifarakano mikubwa
ndani ya chama na kupelekea kuvuliwa uongozi kwa viongozi mbalimbali
katika mkoa wetu kwa maamuzi yasiyo zingatia utafiti na uhalisia wa
kweli ndani ya chama.
Mwenyekiti na katibu mkuu wamekuwa vinara wa kuvunja katiba Mfano:
• Kitendo cha kutoa muongozo nje na
matakwa ya katiba juu ya kuwapata wawakilishi kwenye vyombo vya maamuzi
kama wabunge kwamba wanaohitaji kugombea 2015 waandike barua makao makuu
na wao ndio watatoa wagombea kinyume na katiba ya chama Ibara 7.2.13
inayotoa taratibu ya kuwapata wagombea, huwo ni uvunjaji wa katiba na
ubakaji wa demekrasia ndani ya chama, sizani kama kuna uhaini zaidi ya
huu swali la kujiuliza hapa, Je, kama leo sisi Chadema hatuheshimu
katiba yetu tuliyoitunga sisi wenyewe itakuwaje siku tukikabidhiwa nchi
yenye watu wenye mawazo na mtizamo tofauti na sisi?. Hatutaki kuamini
kama nchi hii inaweza kugeuka uwanja wa maopambano ya kivita.
Tunataka kujua hatua gani zilizochukualiwa
dhidi ya Mbunge wa Arusha Mjini Mh: Godbless Lema kumkashfu kiongozi wa
chama Mh: Zitto Zuberi Kabwe kuwa ni mnafki na Mzandiki kwendye mitandao
ya kijamii pia tunataka kujua hatua gani zilizochukuliwa na chama dhidi
ya Bw Henry Kilewo kwa kuweka waraka unaoitwa ripoti ya siri
inayomhusu Zitto mbao chama makao makuu kupitia kwa mkurugenzi wa habari
na uenezi wa chama kukana mbele ya vyombo vya habari kuwa waraka huo
chama hakiusiki nao na hakiujui kabisa lakini chakushangaza Bw Kilewo
ambaye pia ni kiongozi wa chama ngazi ya mkoa wa Kinondoni kichama,
waraka huo ambao chama kiliukana yeye aliweka kwenye Blog yake ilihali
akijua kufanya hivyo ni kinyume na kanuni za viongozi wa chama kuhusu
maadili ya viongozi kanuni ya 10.
Pia tunataka kujua hatua gani
zilizochukuliwa kwa waandaaji wa tamthilia hii ijulikanayo kama Ripoti
ya siri kuhusu Zitto kwasababu tayari makada na viongozi wetu
wamelidhihiri kuwa wao ndo miongoni mwa waandaaji wa tamthilia hii.
Lakini cha ajabu viongozi wetu wamelifumbia
macho na kupelekea kwetu baadhi ya wanachama kuamini zengwe hili la
kumchafua Zitto Lina Baraka zote za viongozi wa chama ngazi ya juu.
Tunataka kuona nguvu iliyotumika kuwaadhibu
Mh: Zitto na wenzake kwa kuandaa waraka ujulikanao kama mkakati wa
mabadiliko 2013 nguvu hiyo hiyo itumike kwa hawa waliotumia njia chafu
ya kuandaa waraka wa kumchafua zitto ambao chama kinawajua na baadhi yao
tumewaweka humu kwenye tamko letu.
Kingine tunataka kwa mara nyingine kwa
viongozi wa chama makao makuu kuwaambia umma wa watanzania ni kwanini
waraka huo huo uinaoitwa warajka wa siri kuhusu Zitto leo viongozi na
wanachama mikoani na kwenye majimbo waraka huo uangawiwa kwa wanachama
na wananchi kwa agizo la makao makuu kama si ubaguzi ni nini?.
Tunaonya na kulaani kitendo cha viongozi
wetu kuendeleza utawala wa kibabe na kupelekea kuhatarisha maisha ya
baadhi ya wanachama na viongozi wanaotofautiana nao kimtizamo mfano:
kumezuka tabia ya baadhi ya viongozi na makada wa chama chetu wasiokuwa
na uwezo wa kujenga hoja jukwaani hivyo kujikuta muda mwingi wa kutumia
maneno ya uchochezi dhidi ya wanachama na viongozi wanaokinzana nao
kifikra na kimtizamo na kuhamasisha wanachama wasiojua itikadi vizuri ya
chama kuwa wawashughulikie na maneno haya yamekuwa yakisemwa hadharani
kwenye mikutano mbalimbali hivyo wananchi wapenda Demokrasia ya kweli
kubaki na maswali magumu kuliko majibu juu ya ukimya wa serikali
kuhusiana na jambo hili.
Hitimisho
Mwekiti na katibu mkuu wajiudhuru mara moja ili kupisha uchunguzi wa mapato na matumizi ya fedha za chama ambazo zinatokana na kodi za wavuja jasho wan chi hii, M/kiti na katibu mkuu watoe ufafanuzi juu ya kuvunja katiba kwa kuondoa kipengele cha ukomo wa uongozi ndani ya chama kutangaza uchaguzi huku mkiwaondoa washindani wenu ni uwoga na ubakaji wa Demokrasia.

Mwisho tunataka maamuzi haya HARAMU kamati
kuu yabatilishwe na mchakato wa kuwavua viongozi hawa nyazifa zao ufuate
taratibu na kanuni kwa mujibu wa katiba tofauti na hapo tarehe
4/12/2013 tutaungana na wapigania Demokrasia kote nchini kufanya
maandamano yasiyokuwa na ukomo mpaka uongozi uliopo utoke madarakani.
Vile vile baada ya tarehe hiyo muhakikishe mnawaamisha wabunge vibaraka wote wa chadema mkoa wa mwanza, wamchukue wenje wakamtafutie jimbo moshi na highness kiwia wamtafutie jimbo HAI na MACHAME hii ardhi ya kanda ya ziwa sio saizi yao na tunataka waondoke mara moja. Kinyume na hapo tutawaondoa huku wakishuhudia kwa macho yao.

Tunamuagiza mbowe na slaa wasithubutu
kukanyaga ardhi hii ya kanda ya ziwa ikiwa bado hawajajiudhuru ama
kubadili maamuzi yao HARAMU haraka iwezekanavyo
Hatuna sababu ya kuendelea kuwa wsatumwa wa fikra ndani ya chama chetu,
Tumekuwa wanyonge kwenye chama hiki vya kutosha, tumedharirishwa kwenye chama hiki vya kutosha, tumeburuzwa na kupuuza kwenye chama hiki vya kutosha,

Sasa sisi wanachadema wa matawi ya mwanza
na kanda ya ziwa kwa ujumla, tunasema kwamba kanda ya ziwa na magharibi
watupo chadema kwa bahati mbaya, tupo humu kama wapokezi na waasisi
wakuu wa chama hiki, tunajivunia uasisi wa wazee wetu kina Marehemu Bob
Nyanga Makani, Marehemu Balozi ngaiza Marehemu Chacha Zakayo Wangwe,
kamanda Zitto Kabwe na sisi wengine wengi.
Vyovyote itakavyokuwa kamwe, hatutaweza kukubali aina yoyote ya upuuzi huu unaoeneawa na kusimamiwa na WAHUJUMU DEMOKRASIA NDANI YA CHADEMA.
Tunashukuru kwa ushirikiano wenu.
Mapambano yanaendelea. CHADEMA VEMA

ROBERT E. GWANCHELE
Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA
0757 084776Mwenyekiti wa umoja wa Matawi ya CHADEMA mkoa wa MWANZA
Mwenyekiti wa Vijana KANDA YA CHAMA ZIWA MAGHARIBI
Mjumbe kamati Tendaji wilaya ILEMELA