Rais wa Marekani Barack Obama mnamo siku ya Jumatano alikiri kuwa alikatazwa kutotumia simu
aina
ya iPhone kwa sababu za kiusalama, hii ilikuja kipindi ambacho alikuwa
akifafanua ni kwa nini wakati mwengine huonekana akitumia simu kubwa
aina ya Blackberry.
“Siruhusiwi
kwa sababu za kiusalama kuwa na iPhone,” Obama alilieleza kundi la
vijana ndani ya White House kwenye tukio la kuhamasisha sheria ya kujali
afya.