Ilidaiwa
kuwa kikwazo kikubwa wanachokutana nacho ni namna ya kumfikia na kigezo
cha dini kwa sababu Lulu hataki kuolewa na muislam kwani hayupo tayari
kubadili dini.
Akizungumza katika mahojiano maalum, mapema wiki hii, mama wa Lulu,
Lucresia Karugila alisema kwa upande wake yupo tayari kupokea mahari
yoyote ilimradi mwanaye awe ameridhiana na mwanaume husika.
“Unajua Lulu ameshakua, mambo ya kumwingilia mtoto kwenye vitu binafsi ni ya kizamani. “Siwezi kupanga mahari, sijui laki nane au laki ngapi. Kiasi chochote ni sawa cha msingi mwanangu awe amekubaliana na huyo mwanaume.
“Hajaniambia kama kuna mtu anataka kuleta mahari,” alisema mama Lulu.
Kwa upande wake Lulu alisema: “Kwa sasa sina wazo la kuolewa ila naweza kuamka kesho nikabadili uamuzi.” Alipoulizwa kama ni kweli atatakiwa kulipiwa mahari ya laki nane alisita kidogo.