MWENYEKITI CHADEMA MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013
KATIBU WA CHADEMA MKOA
S.L.P 260
SINGIDA
YAH: - KUJIUZURU UENYEKITI MKOA SINGIDA
Somo hapo lahusika,
Ninapenda
kukuarifu kuwa nimeamua kujiuuzuru nafasi yangu ya uenyekiti wa mkoa
ambayo nimekuwa nikiitumikia kwa kipindi kirefu sasa kama kielelezo cha
kuamini na kudai demokrasia ya kweli ndani ya chama.
Ikumbukwe
kwamba mimi ndio mwanachama wa kwanza kujiunga na CHADEMA mkoa wa
SINGIDA na ni mwanachama wa 300 kitaifa, hiyo ni heshima kubwa sana
kwangu na sipo tayari kuipoteza kwa kukubali kuwa sehemu ya
udharirishaji huu wa demokrasia uliopitiliza
Maamuzi
na vitendo vinavyoendelea ndani ya chama chetu kwa sasa ni ubakaji na
udharirishaji wa demokrasia ya kweli tunayoihubiri mbele ya umma.
Kwa
barua hii basi, nimeonelea bora upate ufahamu huo kuwa si vema mimi
kuendelea kupingana na dhamira yangu inayonituma kuwa mwanademokrasia wa
kweli.
Kwa kipindi hiki kifupi mnaweza mkaendelea kuitumia anuani yangu ya posta mpaka hapo mtakapopata anuani yenu tayari.
Ninatanguliza shukrani zangu za dhati kwa wanachadema wote wanaopinga upuuzi huu uliofanywa na kamati kuu ya chama.
Kusimamia
haki, katiba na misingi ya chama ni wajibu wangu, hivyo kwa namna
yoyote ile sitaweza kuwa tayari kufumba macho pindi ujinga wa namna hii
unapoendelea kutekelezwa kwa uwoga wa uchaguzi.
Nakutakia kila la heri kwenye majukumu yako.
………………………………………………….
Wilfred N. Kitundu
MKOA SINGIDA
S.L.P 260
3.12.2013