Search in This Blog

"MIMI NITAKUWA MSTARI WA MBELE KWENYE MAANDAMANO NITAKAYOYAANDAA KUPINGA KUPANDA KWA UMEME" GODBLESS LEMA

MBUNGE wa Arusha Mjini, Godbless Lema ameiomba serikali kutopandisha bei ya umeme kwa ongezeko la asilimia 68, na endapo itakuwa hivyo ataongoza maandamano jijini hapa kupinga hatua hiyo.
Aliyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini hapa wakati alipokuwa akiwahutubia mamia ya wananchi wa jimbo lake, katika mkutano wa hadhara aliouandaa kwa lengo la kuzungumza nao. 
Mbunge Lema alisema inasikitisha kuona baadhi ya viongozi wenye dhamana, wanasema iwapo mwananchi atashindwa kutumia umeme anaruhusiwa kutumia kibatari. 
"Hii lugha si ya kiongozi na inapaswa kupingwa na kila mtu, kwani hatuhitaji ongezeko la gharama za umeme, bali tunahitaji kupunguziwa," alisema Lema. 
Aidha alitoa mfano wa nchi jirani ya Kenya kuwa, serikali kwa kuhurumia wananchi wake, imepunguza bei ya umeme kwa asilimia 12, jambo ambalo lingepaswa kuigwa na serikali ya Tanzania. 
Alisema Tanesco wanataka kupandisha bei ya umeme huku kukiwa na wananchi waliolipia ghrama za umeme ili uwake majumbani mwao bado hawajaunganishiwa umeme huo. 
Aliwasihi Tanesco kuunganisha umeme kwa wananchi ili nao waweze kupata mwanga badala ya hivi sasa kufikiria tu suala la kupandisha bei ya umeme.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger