Kuna familia moja imejengea karibu
kabisa na kwangu tokea wamehamia ni miezi minne na zaidi, Baba wa
familia hii ni wa rika langu kabisa, siku chache baada ya kuhamia
tulikutana kwenye Ibada ya Jumuia mtaa wa tatu, basi tukawa tunaongea
kwa kutaniana akiniuliza wenyeji huwa mnanywea bia wapi? Mimi
nikamshauri kwamba Wikiend tutafutane akiwa anasikia hata mkewe.
From there onward inapotokea mmoja wetu
amekaa sehemu anapata kinywaji tunashtuana na kama upo interested
una-join au unapotezea na mara nyingi tumekuwa tukikutana baadhi ya
Weekends au public holidays.
Majuzi nilikuwa na Business moja ya
kumshirikisha, tukakubaliana tuonane Lunch time kwasababu wote tunafanya
kazi mjini, Kutokana na mda wa Lunch kuwa tight kidogo tulishindwa
kupata mda wa kuzungumza kwani kulikuwa na marafiki wengine ambao
isingekuwa vema wasikie mambo yetu, hivyo tukakubaliana tukutane Jioni
Bar moja ya karibu mtaani kwetu.
Mida ya saa moja na nusu usiku
tukakutana na jamaa na tukaanza mazungumzo, tukiwa kati kati ya
mazungumzo jamaa akawa busy sana na simu ya mkononi kwani alikuwa kila
baada ya dakika chache ananyanyuka kwenda kuongea na simu alafu akirudi
'mudi' yake inabadirika, sikutaka kumuuliza maana niliamini ni mambo
yake binafsi na ndomaana hakutaka nisikie anaongea nini.
Baadaye jamaa akazima simu yake,
tukaendelea na mazungumzo huku tukipata Bia mbili tatu, ilipofika saa
tatu na dakika kadhaa usiku nikapigiwa simu na namba ambayo sikuwa
nimei-save, nikasikia sauti ya mdada lakini siku-notice ni nani,
akajitambulisha kwamba yeye alikuwa ni mke wa Jamaa niliye naye Bar
akaniuliza kama kweli nipo naye nikathibitisha hilo, Hapo ndipo
alipoanza kunishambulia kwamba tokea nimefahamiana na mmewe, mmewe
amekuwa akichelewa kurudi nyumbani, na ameanza tabia ya Umalaya, hivyo
akaniasa niache kumfundisha mmewe Tabia zangu chafu za umalaya.
Nimeumia sana kwasababu hata siku moja
huwezi ukamfundisha tabia mbaya mtu mzima mwenzako, labda na yeye awe
tayari anatabia hizo, huo umalaya wangu sijui kaufahamia wapi kwasababu
hatujawahi kufahamiana kabla ya wao kuhamia mtaani, japokuwa wife
kasafiri mda mrefu nimejitahidi sana kujizuia na haya mambo, na mbaya
zaidi wife akirudi akikuta sipo katika mahusiano mazuri na Mke wa jirani
ata-draw picture gani? Nifanye nini ili tuendelee kuheshimiana na huu
dada? Napata taabu kwasababu nikimueleza mmewe kwamba aangalie cha
kufanya ili mkewe afute imani mbaya aliyo nayo juu yangu lakini jama
-Jamii Forums