Imezoeleka
kuona Simba pekee ambao wanaweza kupanda juu ya Miti ni kutoka hifadhi
ya Taifa ya Manyara, lakini hata hivyo kulikuwa hapajajulikana ni
hifadhi ipi nyengine ambayo Wanyama hao waliweza kuonekana wakiwa Juu ya
miti..
Hivi
karibuni mtandao wa Maliasili zetu wakati wa safari zake za kutembelea
baadhi ya hifadhi za Taifa ulibaini kuwapata Simba wengine katika Mbuga
ya wanyama ya Mikumi wakiwa juu ya Miti.
Simba hao
ambao walikuwa ni majike walikuwa wamepanda juu ya mti na kuanza
kucheza huko kwa muda wa masaa zaidi ya mawili ambapo waliwaduwaza
watalii wengi na kuwaacha waendelee kuwashangaa na kukatisha safari zao
ambazo walikuwa wazifanye kwa masaa yote hayo mawili. ...
Hivi ndivyo ilivyo kuwa ...
Watalii wakiwashangaa Simba hao (HD) JIUNGE NA UKURASA WETU WA FACEBOOK KUPITIA HAPA >>MDADISI MAMBO