Search in This Blog

PADRI MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUTOMTUNZA MTOTO ALIYEZAA NA MHUDUMU WA KANISA

Catholic-Church 75136
PADRE wa Kanisa Katoliki Singida mjini Deogratus Makuri amefikishwa mbele ya mahakama ya mwanzo Utemini mjini hapa akituhumiwa kushindwa kutunza mtoto wake wa kike.
Ilidaiwa mahakani hapo, kuwa Padre Makuri alikuwa na uhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na Maria Boniphance (26) mkazi wa Mitunduruni mjini hapa na mhudumu katika parokia ya Singida mjini.(HD)
Ilidaiwa mbele ya hakimu wa mahakama hiyo,Ferdnand Njau kuwa katika muda huo wa mahusiano ya kimapenzi ndipo mdaiwa Makuri alipompa ujauzito Maria.
Maria aliiambia mahakama hiyo kuwa mara tu alipopata ujauzito huo alilifikisha tukio hilo kwa wazazi wake.
Amesema wazazi wake walimwendea na bila kuuma ulimi alikubali kumpa uja uzito Maria na kuahidi kwa maandishi kuwa atamtunza mtoto wake (jina tunalo) hadi hapo atakapokuwa na uwezo wa kujitegemea.
Maria amesema Padre ambaye inadaiwa kwa sasa amesimamishwa wadhifa wake huo kutokana na tuhuma hiyo, alitekeleza ahadi yake hiyo kwa miezi michache na kisha kugoma kuendelea kutoa matunzo.
"Baada ya hapo nilimfikisha mbele ya ofisi ya ustawi wa jamii ambapo katika hati ya mkataba, aliahidi kuwa atakuwa anatoa kila mwezi shilingi 80,000/= na endapo atashindwa kutekeleza ahadi hiyo,aliomba afikishwe mahakamani mara moja",amesema.
Ilidaiwa kuwa pamoja na ahadi hiyo nzito,Padre Makuri alianza kudai kwamba mtoto huyo sio mtoto wake wa kuzaa na kisha kuacha kutoa matunzo kama alivyoahidi.
Katika hatua nyingine,Maria amesema walianza mapenzi siku Padre huyo kumpa kazi ya kufanya usafi kwenye kabati la vitabu chumbani kwakewakati akiendelea kufanya usafi alifungiwa kwa nje hadi hapo usiku aliporejea Padre akiwa na chakula cha jioni cha mhudumu Maria.
Amesema Padre alimwambia kwa vile umekuwa ni usiku alale humo ndani na Padre na kitendo hicho ndicho kilichoanzisha safari ya mahusiano yao ya kimapenzi na kupelekea wapate matunda ya kuwa na mtoto.
Habari zaidi kutoka kwenye parokia hiyo zinadai kuwa Padre Makuri alikuwa kwenye maandalizi ya kwenda kuongeza elimu nje ya nchi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger