Alisema kuanzia leo,
watumishi wote waliopo chini ya Wizara hiyo watapaswa kuwasilisha vyeti vya
vyuo walivyosomea.
"Natoa mwezi mmoja kuanzia leo hadi Januari, wawasilishe vyeti vyao wizarani viweze kukaguliwa...baada ya ukaguzi tutafuatilia maeneo waliyosomea ili kubaini kama kuna askari wanaotumia vyeti feki," alisema.

Alisema askari ambao
watabainika kutumia vyeti feki na kupata vyeo wakiwa kazini, watashushwa vyeo
ambapo lengo la ukaguzi huo ni kuwataka watumishi hao kusomea katika vyuo
vinavyotambulika na Serikali si vya mitaani.
Aliongeza kuwa, mpango
huo pia utawahusisha watumishi ambao wamesomeshwa na Wizara ambao nao
watatakiwa kuwasilisha vyeti vyao upya.Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa
SSRA, Bi. Irene Isaka, aliwataka watumishi wa Wizara hiyo kujiunga na Mifuko ya
Hifadhi za Jamii kwa ajili ya kuweka mafao yao.
Alisema kuna mifuko
mingi hivyo kila mtumishi anaweza kuchagua wowote anaopenda kujiunga nao ili
uweze kumsaidia dhidi ya matukio yasiotarajiwa. Matukio hayo ni pamoja na
maradhi, ulemavu, kustaafu kazi,kuacha kwa hiari au kwa lazima.
Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.
-MAJIRA
Akizungumzia changamoto zilizopo katika sekta hiyo, alisema takwimu zinaonyesha wananchi walio katika sekta rasmi wanakadiriwa kufikia milioni 1.5 ndio wananufaika na sekta hiyo.
-MAJIRA