Mkurugenzi
wa Masoko wa Kampuni ya LG Electronics wa Afrika Mashariki, Moses Marji
(kushoto), Mtafiti katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi
na Tiba cha Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala na Meneja Masoko wa LG,
Soyoung Lee, wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa viyoyozi vya
kufukuza mbu viitwavyo ‘LG Mosquito Away’ jijini Dar es Salaam leo.
Mtafiti
katika Idara ya Vijidudu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Tiba cha
Muhimbili (MUHAS), Dk Billy Ngasala akihojiwa na waandishi wa habari
muda mfupi baada ya uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuza mbu viitwavyo LG
Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi
ya watu waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa viyoyozi vya kufukuzia mbu
vya LG Mosquito Away jijini Dar es Salaam leo. Viyoyozi hivyo vinatumia
mawimbi ya kielektroniki kufukuza mbu waenezao ugonjwa wa malaria