Na Shakoor Jongo
STAA wa sinema za Bongo, Jacqueline
Wolper amemrushia maneno ya lawama Mtangazaji wa Kipindi cha Take One,
Zamaradi Mketema kuwa ni mnafki na adui yake mkubwa katika maisha.
Akizungumza na Amani juzikati, Wolper
alisema amegundua kuwa mtangazaji huyo amekuwa akimfuatilia kwa karibu
sana maisha yake kwa mtindo wa chanya (negative), akamuomba amuache.
“Nilibadili dini kutoka Ukristo kwenda
Uislamu, Zamaradi akanifuatilia, juzijuzi nimerudi kundini (kwenye
Ukristo) kwa kusikiliza maneno ya wazazi wangu, akanifuatilia tena.
“Huko nyuma kupitia kipindi chake
alikubali nidhalilishwe na waigizaji wenzangu kwa faida yake (hakutaka
kufafanua), iliniuma sana. Leo (hivi karibuni) kaniweka hewani (kwenye
redio) bila ya ridhaa yangu. Naomba niseme kuwa naanza kugundua azma
yake kwangu ni nini, aniache na maisha yangu,” alilalama Wolper.
Baada ya Wolper kulalamika sana, Amani
lilimtafuta Zamaradi kwa njia ya simu ya kiganjani ambapo alisema yeye
anawajibika kwa kazi yake hakuna ishu ya kumfuatilia mtu.
“Mimi
simfuatilii maisha yake, ni kazi tu. Kama mwandishi wa habari nikipata
habari ya mtu natakiwa kubalansi (uwiano) naye,” alisema Zamaradi.
GPL