Search in This Blog

MKUTANO WA BONGO MOVIES NA BONGO FLEVA TIMBWILI LAIBUKA

JAZBA baab’kubwa imeibuka katika mkutano wa wasanii wa filamu za Bongo ‘Bongo Movies’ na Bongo Fleva ulioandaliwa na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa kushirikiana na chombo cha kusimamia haki za wasanii nchini, Cosota.

 

Jacob Steven ‘JB’.

Tukio hilo lilijiri Jumatatu iliyopita ndani ya Ukumbi wa Vijana Social, Kinondoni, Dar ambapo mastaa wa filamu, Jacob Steven ‘JB’ na Issa Mussa ‘Cluod 112’ waliihoji Cosota juu ya tatizo la wizi wa kazi za wasanii ndipo ‘kiliponuka’ baada ya kutoridhishwa na majibu.
Issa Mussa ‘Cluod 112’.
Hali hiyo ilisababisha baadhi ya wasanii, wakiwemo JB na Cloud kutoka kikaoni na kuendelea na mambo yao mengine huku wawakilishi wa TRA wakiendelea na kikao na kufafanua mipango yao.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger