Search in This Blog

MUONE MKALI WA KURUKA NA PIKIPIKI JUU YA MOTO MKOANI MROGAOA


Mengi Ngadu maarufu kama lion akiruka na pikipiki aina ya Yamaha DT Sport 125 kuruka moto wakati wa bonanza la mashindano ya Endula 2014 ya kukaribisha mwaka mpya na kuaga mwaka 2013 katika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Morogoro.


MWENDESHA pikipiki za michezo wa klabu ya Ruaha Motor Cycle wilaya ya Kilosa, Mengi Ngadu ameibuka mshindi wa kwanza wa bonanza la Endula la mashindano ya pikipiki la kuukaribisha mwaka mpya 2014 na kuaga mwaka 2013 lililofanyika uwanja wa Sabasaba Manispaa ya Moroogoro.


Katika mashindano hayo yaliyoshirikisha waendesha pikipiki za michezo sita kutoka klabu tatu za Mikumi Motor Cycle, Ruaha Motor Cycle na wenyeji Morogoro, Morogoro Motor Cycle yalipokewa kwa shangwe na mashabiki wa mchezo huo waliofurika kwenye uwanja huo wa Sabasaba.


Akizungumza na mwandishi wa habari hizi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Mratibu wa bonanza hilo, Hussein Makusi alisema kuwa Mengi Ngadu ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza hasa baada ya kufanikiwa kuruka vizuri kiunzi chenye moto.


Makusi alisema baada ya Ngadu kushika nafasi ya kwanza kwa kuruka kiunzi chenye moto nafasi ya pili ilichukuliwa na Ally Ramadhan (17) aliyefanya vizuri katika mbio za mwendo kasi na kukwepa vizingiti wakati nafasi ya tatu ilikwenda kwa Hamis Mdeng’o.


“Mashindano ya Endula ni mashindano ya ndani ya uwanja na na tulikuwa na washiriki sita yenye ikihusisha michezo mitatu ikiwemo ya kuruka kiunzi cha moto, kukimbia kwa kwendo kasi na kukwepa vikwazo na kuonyesha umahili wa namna ya kucheza na pikipiki”. Alisema Makusi.


Aliwataja walioshiriki bonanza hilo kuwani ni Yahaya Awezo, Rashid Ramadhan, Abdul Ngwage na Hamis Mdeng’o kutoka klabu ya Morogoro Motor Cycle huku Ruaha Motor Cycle ikiwakilishwa na Mengi Ngadu na Maulid Hamad (30) akitoka klabu ya Mikumi Motor Cycle.


Mshindi wa kwanza alitarajiwa kuibuka na kitita cha sh100,000 huku mshindi wa pili akichukua sh50,000 wakati yule wa tatu akipata zawadi ya sh30,000.


Naye mashindi wa bonanza hilo, Mengi Ngadu maarufu kama Lion alisema kuwa amekuwa akikabiliwa na changamoto kubwa wa upatikanaji wa vifaa vya mchezo huo ikiwemo pikipiki ya michezo.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger