Mtu mmoja asiyefahamika jina anayedaiwa kuwa ni mwanga amenaswa na polisi baada ya kudondoka katika eneo la Ilala Bungoni, jijini Dar akiwa kama alivyozaliwa.
Tukio
hilo lilitokea Jumamosi iliyopita kuamkia Jumapili saa kumi usiku
wakati mtu huyo alipodaiwa kudondoka akiwa na ungo, hirizi na
kusabababisha watu waliokuwa eneo hilo kutahamaki.
Chanzo
chetu kimesema kuwa, mara baada ya mtu huyo kudondoka watu waliitana na
kukusanyika na wengine kutoa taarifa jeshi la polisi kwa njia ya simu
ambao walifika haraka.Watu waliokuwa katika eneo hilo walishangaa kuona mtu wa namna hiyo ametokea kusikojulikana na kuanguka na vitu ambavyo inadaiwa ni vya kiuchawi.
Askari
polisi waliofika eneo la tukio walifanya kazi ya ziada kuzuia watu
waliokuwa na lengo la kumpiga mtu huyo aliyeonekana kutojitambua kwa
madai kuwa ni kwa sababu ya kudondoka kutoka angani.
“Hili
ni tukio la kwanza kutokea hapa na limetushangaza sana, tunaamini kuwa
alidondoka kwa sababu tulisikia kishindo na tulipokuja kuangalia ni nini
tukamkuta mtu huyu akiwa na hirizi, ungo na tunguri, alitueleza kwa
tabu kuwa alikuwa na wenzake,” alisema shuhuda mmoja aliyejitambulisha
kwa jina la Juma Hussein.
Naye Asha Hamisi alisema mtu huyo wamaamini kuwa ni mwanga kwa kuwa alikuwa na vitu vinavyofanywa na wachawi au waganga.