Search in This Blog

USHAURI: “NIMEZAA NA DADA YANGU WA DAMU, NIFANYEJE”

Moja kwa moja niende kwenye maada. Mkasa huu umenikumba nikiwa nafanya kazi mkoa flani kanda ya kati. Katika eneo ambalo nilikuwa naishi ni karibu na sehemu ambayo baba yangu alikuwa anafanyia kazi kabla ya kustaafu na kurudi nyumbani kwake namaanisha mkoa alikozaliwa yeye ambao upo kusini nyanda za juu. 
 
Wakati baba anastaafu na kurudi mkoa aliozaliwa mimi na nikabaki mkoa huo huo aliokuwa anafanya kazi sikuweza kuhama naye kwasababu nilikuwa nafanya kazi kwenye kampuni moja ya mawasiliano .
 
Katika kipindi alichokuwa anafanya kazi kumbe alizaa nje ya ndoa na mwanamke mmoja lakini baba hakuweza kumhudumia yule mtoto kitendo ambacho kilimfanya mama mtoto asimweke karibu na baba.
SAD
Hata yeye baba hakuwahi kutuambia kuwa aliwahi kuzaa nje ya ndoa. Katka kipindi chote hicho mama huyo na mwanaye walikuwa wakiishi mbali kidogo na wilaya yetu.
 
Basi katika mizunguko ya kazi hapa na pale nilikutana na dada huyu ambaye ndiye nimezaa naye pasina kujua ni dada yangu. Tulikutana kwenye semina mkoani Kilimanjaro kama ilivyo kawaida ya wanaume nikamuaproach yule dada na akaingia line. Tukaanza kujihusisha kimapenzi kwa muda wa mwaka mzima mpaka alipopata ujauzito.
 
Ikanilazimu niukubali ule ujauzito na nikatafuta wazee wa mtaa ninaokaa na kwenda nyumbani kwa mwanamke ili kujitambulisha. Yule mama mkwe ambaye ni mama mdogo kihalali alipoona majina yangu matatu akapatwa na wasi wasi japo barua ilipokelewa.
 
Ikabidi akanitafuta kwa kuniuliza kiundani nilipojieleza ndipo akasema huyu uliyempa mimba ni dadayako tena wa damu. 
 
Kwakweli niliishiwa nguvu akaanza kunisimulia kila kitu kuhusu baba yangu. Mpaka hapa ninapo andika mwanamke ameshajifungua na mtoto ana miezi 5.
 
Baba sijamwambia bado ila nataka nimpeleke huyu binti nyumban kwetu. Na hii siri naijua mimi na mama mkwe au mama mdogo. 
 
Sijajua nifanyeje mama mwenyewe ameshindwa afanye nini, tunaogopa kuwashirikisha watu aibu.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger