ANGALIA TRAILER YA MOVIE MPYA MAALUM KWA KANUMBA 'AFTER DEATH'
Baada ya kutimia Mwaka mmoja sasa toka alipoondoka duniani msanii mahiri
wa bongomovie, Marehemu Steven Kanumba, Msanii mwenzake Jack Wolper
aamua kufanya movie kwa ajili ya kumuenzi star huyo, movie
itakayozinduliwa hii leo katika viwanja vya leaders club maalumu kwa
ajili ya kumuenzi na kumkumbuka marehemu. Kitu kizuri katika hii movie
ni kuwapo kwa kijana ambaye ameact kama mdogo wake Kanumba, ambaye
ameitendea haki sana nafasi aliyopewa kuact kwani ameact kama Kanumba
alivyokuwa akicheza, NSIKUNYIME uhondo kwa stori nyingi, Icheki trailer
ya movie hii hapa then toa maoni yako unaionaje?
No comments:
Post a Comment