Search in This Blog

ZANZIBAR YAPINGA MARUFUKU NDOA YA JINSIA MOJA

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imetunga sheria ya kupiga marufuku ndoa za watu wa jinsia moja.
Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar, Bwana Abubakar Khamis Bakar, aliyasema hayo kwenye Kikao cha Baraza la Wawakilishi Zanzibar wakati akijibu swali la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi, Saleh Nassor Juma kutoka Chama cha Wananchi (CUF).


Mhe. Abubakar Khamis Bakar, Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar
                                                   Mhe. Abubakar Khamis Bakar, 
                                          Waziri wa Katiba na Sheria wa Zanzibar

Katika swali lake, Bw. Saleh Nassor Juma alitaka kujua ni lini Serikali ya Zanzibar itatunga sheria ya kukataza ndoa hizo na kuweka adhabu kali kwa watu ambao watabainika kufanya vitendo hivyo vichafu.
Waziri Abubakar amesema, ndoa za watu wa jinsia moja ni kinyume na utamaduni wa Zanzibar na kwamba sheria hiyo imeweka adhabu ya kifungo cha miaka saba kwa wale wote watakaopatikana na hatia hiyo.
Pia alisema kama ninavyomnukuu: "Sheria hii inahusu makosa mengi yakiwemo ya ubakaji, zinaa, usagaji na umalaya ambayo yote yana adhabu ya kifungo cha maisha au miaka isiyopungua 30 gerezani," mwisho wa kunukuu.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger