Search in This Blog

"BODABODA ZAUA LAKINI HATUWEZI KUZIZUIA" WAZIRI MKUU


Ni kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda aliyoitoa bungeni alipojibu maswali ya wabunge.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda amesema si rahisi Serikali kupiga marufuku usafiri wa pikipiki kubeba abiria maarufu kama bodaboda licha ya kutambua kuwa ni sababu kubwa ya ajali na vifo vya watu wengi.Badala yake, Pinda alisema kinachofanyika ni kutoa elimu kwa kutumia vyombo mbalimbali hadi vijijini walikosambaa, kwa kuwatumia polisi, vyuo vya Veta na asasi za kiraia ili kupunguza ajali hizo.Kipindi cha mwaka jana pikipiki ziliua watu 771 kwa ajali 4,637 ambapo watu wengine 4,562 walijeruhiwa.                             
Mwaka 2011 ajali za pikipiki zilikuwa 3,326 na kusababisha vifuo vya watu 594 na kujeruhi wengine 3,034.Pamoja na ajali hizo, Pinda alisema Serikali inashindwa kuzisimamisha pikipiki kwa sababu kwa upande mwingine zinasaidia.Pinda alitoa majibu hayo wakati anajibu swali la Magdalena Sakaya (Viti maalumu-CUF) aliyetaka kujua tamko la Serikali kuhusu usafiri huo ulioruhusiwa nchini kwa sheria ya Bunge lakini matokeo yakawa kinyume na matarajio.
Kwa mujibu wa Sakaya, badala ya kuleta neema iliyotarajiwa usafiri huo umegeuka balaa kwa kusababisha vifo na ulemavu wa vijana wengi nchi nzima.Alisema waendeshaji wa pikipiki wengi hawafuati sheria, ni wajeuri hivyo akapendekeza wapewe kozi ya miezi mitatu ili kuwaweka sawa.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger