
Mshukiwa wa mauaji aliyehukumiwa kifo nchini Iran
Juhudi za kukomesha hukumu ya
kunyongwa duniani zinaendelea katika baadhi ya nchi licha ya nchi
kadhaa kuanza tena kutekeleza hukumu hiyo mwaka 2012. Hii ni kulingana
na shirika la Amnesty International.
Utekelezaji wa hukumu hiyo ulitokea nchini
India, Japan, Pakistan na Gambia, na hili lilikuwa jambo la kusikitisha
kulingana na Amnesty.Nchi tano ambazo zimeripotiwa kutekeleza hukumu hiyo pakubwa, ni pamoja na China, Iran, Iraq, Saudi Arabia, na Marekani
Amnesty International imeelezea kuwa na wasiwasi kuhusu ongezeko la visa vya watu kunyongwa nchini Iraq - huku idadi ikiwa kubwa zaidi mwaka jana ikilinagnishwa na mwaka 2011 kutoka 68 hadi 129.
Shirika hilo liligindua kuwa nchini Iran mnamo mwaka 2012 takriban watu 314, walinyongwa nchini na wengine 79 nchini Saudi Arabia.
Marekani iliwanyonga watu 43 idadi sawa na walionyongwa mwaka 2011, ingawa katika majimbo machache .
Hata hivyo, hakuna idadi kamili ya walionyongwa inajulikana nchini China ambako kuna usiri mkubwa.. Hata hivyo shirika hilo linaamini kuwa maelfu ya watu walinyongwa, ikiwa idadi kubwa zaidi kuliko katika nchi yoyote duniani.
Aidha shirika hilo liligundua kuwa visa vya kutekeleza hukumu ya kunyongwa vinashuka chini kote duniani licha ya idadi ya nchi zinazoanza kutekeleza hukumu hiyo.
India imetekeleza hukumu yake ya kwanza tangu mwaka 2004, dhidi ya mshukiwa pekee aliyesalia wa mashambulizi ya mwaka 2008 mjini Mumbai.
Nchini Indonesia ambako, mwanamke muingereza Lindsay Sandiford, anakabiliwa na hukumu ya kunyongwa kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya, pia imetekeleza hukumu yake ya kwanza ya kunyongwa katika kipindi cha zaidi ya miaka minne.
Hata hivyo hili halikujumuishwa katika ripoti ya shirika la Amnesty.

chanzo: http://www.bbc.co.uk
No comments:
Post a Comment