Arusha. Mtu mmoja ameuawa kwa kupigwa risasi na
wengine wawili wamejeruhiwa, akiwamo askari polisi, baada ya majambazi
kuvamia gari lililokuwa limebeba Sh58 milioni zilizokuwa zinapelekwa
benki.
Tukio hilo lilitokea jana saa 5:30 asubuhi katika
eneo la Idara ya Maji, katikati ya Jiji la Arusha na kuzua tafrani ya
aina yake, baada ya majambazi hao kupiga risasi ovyo hewani kabla ya
kupora kiasi hicho cha fedha.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Kamishna
Msaidizi wa Polisi, Ibrahim Kilongo alithibitisha kutokea kwa mauaji na
uporaji huo wa fedha za Kampuni
ya Mafuta ya Panone.
Kamanda Kilongo, alisema majambazi hayo yakiwa na
pikipiki, yalivamia gari lililokuwa likiendeshwa na Moses Masania, akiwa
na wahasibu wawili Hapiness Ndasai na Jacline Dastin wa kampuni hiyo.
Alisema majambazi hayo yaliyokuwa matatu,
yakitumia pikipiki, yalizuia gari hilo kwa mbele eneo la Idara ya Maji
na kuvunja kioo cha mbele cha gari na kisha kumpiga risasi Masania
ambaye alifariki papo hapo. ya Mafuta ya Panone inayomilikiwa na Patrick
Olomi. Kamanda Kilongo, alisema majambazi hao wakiwa na pikipiki,
walivamia gari lililokuwa likiendeshwa na Moses Masania, akiwa na
wahasibu wawili Hapiness Ndasai na Jackline Dastin wa kampuni hiyo.
Alisema majambazi hao waliokuwa watatu, wakitumia
pikipiki, walilizuia gari hilo kwa mbele eneo la Idara ya Maji na
kuvunja kioo cha mbele cha gari na kisha kumpiga risasi Masania ambaye
alifariki papohapo.
Kamanda Kilongo alisema katika vurugu hizo za
uporaji, majambazi hao pia walimjeruhi kwa risasi Hapiness na askari
polisi Koplo Kudura aliyekuwa njiani katika shughuli zake.
“Wote walipata majeraha kidogo, na polisi
aliyepigwa risasi mguuni alitibiwa na anaendelea vizuri,” alisema
Kamanda Kilongo. Alisema katika tukio hilo majambazi hao walifanikiwa
kutoweka na fedha Sh58 milioni zilizokuwa zinapelekwa benki.
Tukio hili limekuja wakati matukio ya ujambazi
yameanza kurejea Arusha, kwani hivi karibuni majambazi walimuua kwa
risasi mfanyabiashara wa madini na kutoweka na madini aliyokuwa nayo.
Kamanda Kilongo ametoa wito kwa wafanyabiashara
wanaobeba fedha nyingi kupeleka benki, watoe taarifa ya kuomba msaada
kwa polisi.
Hata hivyo, alisema hadi kufikia jana jioni msako wa kuwakamata majambazi hao, ulikuwa unaendelea.