Msafara wa mkuu wa
wilaya ya Handeni Muhingo Rweyemamu wapapata ajali,wawili wapoteza maisha na
wengine wajeruhiwa vibaya
Ajali
hiyo imehusisha gari la Halmashauri ya wilaya ya Handeni ambapo watu wawili
wamefariki akiwemo mwandishi wa Habari Hamis Bwanga na Afisa uhamiaji wa
wilaya.
Watu
wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea majira ya saa 4.30 leo asubuhi
katika kijiji cha Misima kweye barabara ya Handeni Korogwe wakiwa kwenye
msafara wa kikazi kwenda vijijini kwaajili ya shughuli za upandaji wa miti
kiwilaya.

Amesema
gari hiyo ya halmashauri imepinduka baada ya kuacha njia na kwenda kama mita
mia ambapo iliparamia jiwe na imeharibika vibaya. Kwa mujibu wa maelezo yake
taarifa zaidi zitapatikana baadae kwani kwa sasa kinachofanyika ni kuwahudumia
majeruhi ambao wanakimbizwa katika hospitali ya rufaa ya KCMC Moshi mkoani
Kilimanjaro na pia kushughulikia miili ya marehemu.
No comments:
Post a Comment