
Msemaji
Mkuu wa Polisi Advera Senso alisema kwamba:
“Ni kweli
kwamba tunaye, tunaendelea kumhoji,
tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”
tunachoomba ni kwamba mtupe nafasi ili tufanye kazi yetu na kukiwa na jambo lolote tutawajulisha.”
Hata
hivyo, Senso hakuwa tayari kueleza kwa undani muda aliokamatwa Mjengwa wala
sababu za kukamatwa na kuhojiwa kwake, lakini chanzo chetu ndani ya Jeshi la
Polisi kilithibitisha kwamba pamoja na mambo mengine kuhojiwa kwake kulihusu
uteswaji wa Kibanda.
Jumatatu
wiki hii, Kaimu Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai Nchini, Issaya Mngulu alisikika
akizungumza na Kituo cha Radio One cha Dar es Salaam kwamba kesho Jumatatu
(April 15, 2013) polisi watatoa taarifa rasmi ya hatua waliofikia katika
upepelezi wa kesi ya Kibanda.
Kwa
upande wake Mia Mjengwa ambaye ni mke wa Mjengwa, alisema mumewe alipata wito
kutoka polisi makao makuu Alhamisi na kwamba juzi Ijumaa alisafiri kutoka
Iringa kwenda Dar es Salaam kuitikia wito huo.
“Ninachojua
ni kwamba aliitwa kwenda polisi na leo (jana) alinipigia simu kama saa 7:00
mchana na aliniarifu kwamba yupo polisi, sasa tangu wakati huo sijaongea naye
tena na wala simu zake hazipatikani,” alisema Mia na kuongeza: “Kwa hiyo mimi
kwa kweli sifahamu kwamba anahojiwa kwa sababu gani.”
Taarifa
za kukamatwa kisha kuhojiwa kwa Mjengwa ambaye pia ni mmiliki wa Mjengwa Blog,
zimekuja siku chache tangu msaidizi wake katika Blog hiyo, Joseph Ludovick
akamatwe, kuhojiwa kisha kufikishwa mahakamani kwa tuhuma za ugaidi.
Ludovick
alifikishwa mahakamani pamoja na Mkurugenzi wa Usalama wa Chama cha Demokrasia
na Maendeleo (Chadema), Willifred Lwakatare wakikabiliwa na tuhuma za ugaidi na
kupanga kumteka Mhariri Mtendaji wa Mwananchi, Dennis Msacky.
Kuteswa Kibanda.
Machi 5,
mwaka huu saa 5.30 usiku, Kibanda ambaye pia ni Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya
Kampuni ya New Habari (2006) Ltd, alinusurika kifo baada ya kuvamiwa na watu
wasiojulikana nyumbani kwake kisha kupigwa na kujeruhiwa vibaya.
No comments:
Post a Comment