Kuna dada mmoja anasoma chuo Buguruni
na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.
Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu
akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa Lugalo hospitali na kumuulizia
habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza
zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda
hapo hospitali na yote yalikuwa kweli.
Na zaidi akamwambia najua sasa hivi
unaelekea chuo Buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni
akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kujua kuhusu hicho chuo hivyo
nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo
dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu
atakuwa anamfahamu vizuri.
Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake
watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,
kupokea yule mtu akamwambia akuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara
na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu
haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu
akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.
Lakini alipomtazama hakumfahamu
kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na
zaidi alijikuta yuko maeneo ya Chuo Kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia
simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote,
kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae
ili kupata msaada ikabidi awahishwe Mwananyamala hospitali lakini
ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo Regency
hospitali, hivyo akawahishwa Regency na kupata matibabu.
Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu
huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa, tigo pesa na bank (NMB na CRDB)
kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password
pasipo kujijua.
Na bank walipotazama kwenye ATM
Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini
polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara
nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu
walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha. Ingawa
polisi wameshindwa kumkamata.
Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu
akampigia simu akimwambia kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa
zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia tutafutie mtu ambae unahisi
ana pesa kuliko hizi halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo
inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye.
JAMANI HEBU SOMENI NA IKIWEZEKANA MPE TAARIFA NA MWENZAKO
No comments:
Post a Comment