Search in This Blog

KAMA KAWA RAISI KIKWETE HUYOOO UHOLANZI

Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete, anaanza ziara rasmi ya Kiserikali ya siku mbili katika Ufalme wa Uholanzi kwa mwaliko wa Malkia Beatrix wa nchi hiyo.

Rais Kikwete akiambatana na Mama Salma Kikwete na ujumbe wake, waliondoka nchini jana mchana kwenda Uholanzi tayari kwa ziara hiyo ambako pia ataandamana na Mawaziri wanne wa Serikali.

Mawaziri hao ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, Waziri wa Viwanda na Biashara, Dk. Abdallah Kigoda, Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Maji, Ardhi, Nishati na Maendeleo ya Makazi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ramadhan Shaaban.

Leo Rais Kikwete atafanya mazungumzo rasmi ya Kiserikali kati ya Tanzania na Uholanzi kwenye Makazi Rasmi ya Waziri Mkuu. Mazungumzo hayo rasmi yatakuwa kati ya Rais Kikwete na ujumbe wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Uholanzi, Frans Timmermans.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger