Search in This Blog

BOSI WA TAARABU AFARIKI DUNIA

MKURUGENZI na mwimbaji mahiri na mpiga kinanda wa kundi la East African Melody, Hajji Mohamed amefariki Dunia leo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Marehemu Hajji Mohamed, enzi za uhai wake.
Habari kutoka ndani ya kundi hilo zinasema kuwa marehemu alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya presha, huku alipofika Hospitalini hapo alikuwa akitembea mwenyewe.

Aidha pia bosi huyo wa East African Molody alikuwa akisumbuliwa na matatizo ya kushindwa kupumua na kusababisha kifo chake

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger