“Kama watu wanasema ni porojo za Shibuda, basi
wasubiri kama hotuba ya Waziri Mkuu haitakuwa na majibu kwa wafugaji,
lazima hayo yatatokea kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu,
hawa nao ni binadamu waambiwe basi kama hawatakiwi Tanzania,”
alisisitiza.
Mbunge huyo alitoa kauli hiyo juzi akiwa na
uongozi wa wafugaji kutoka Kanda ya Ziwa ambao wako Dodoma kwa lengo la
kuonana na Mawaziri wa Maliasili na Mawaziri wa Mifugo akiwemo Waziri
Mkuu, ili kufikisha kilio cha wafugaji ambao wanateketezewa mifugo yao
na askari wa wanyama pori.
Shibuda alisema kuwa “Katika nchi yoyote duniani
hakuna mateso yanayofanywa kwa wananchi wake kama ambavyo inafanyika
Tanzania kwa upande wa wafugaji, ni heri ya wakimbizi watakuwa na amani
kuliko hawa wanaonekana kama takataka.”
No comments:
Post a Comment