
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry, akijibu maswali kutoka
kwa waandishi wa habari nchini China alipofanya ziara juzi.Picha na
AFPAFP
Waziri wa Mambo ya Nje John Kerry aamua kutafuta muafaka kupitia nchi ya China
China. Waziri wa Mambo ya Nje wa
Marekani, John Kerry, amewasili nchini China, katika juhudi za
kuishawishi nchi hiyo kuishinikiza Korea Kaskazini kusitisha mpango wake
wa nyuklia.
Akiwa nchini humo Kerry alisema China na Marekani wana lengo moja la kusuluhisha mzozo wa kinyuklia wa rasi ya korea na kuitaka Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo ya kimataifa.
Akiwa nchini humo Kerry alisema China na Marekani wana lengo moja la kusuluhisha mzozo wa kinyuklia wa rasi ya korea na kuitaka Korea Kaskazini kurejea katika meza ya mazungumzo ya kimataifa.
Kerry alifanya mazungumzo na Rais Park Geun-Hye na
kuahidi msaada wa Marekani katika mipango yake ya kuanzisha nia ya
kufanya mazungumzo na majirani zake ili kutuliza hali ya wasiwasi
inayoongezeka.
Katika mkutano wake na maofisa wa chama tawala
uliofanyika jana, Rais Park amesema Korea Kusini inapaswa kukutana na
Korea Kaskazini, ili kusikiliza nchi hiyo.
Wakati Kerry akiionya Korea Kaskazini kuachana na
mpango wa kufanya jaribio la kombora, na kwamba nchi hiyo haiwezi
kukubalika kama taifa lenye nguvu ya nyuklia, kufanya hivyo nchi hiyo
itakuwa imefanya kosa kubwa.
Kerry alisema Rais Park alichaguliwa kwa misingi
tofauti ukiwemo uwezekano wa kuleta amani na kwamba Marekani inaheshimu
hali hiyo.
Alisema wamejiandaa kufanya kazi kwa imani kwamba uhusiano kati ya Korea Kusini na Korea Kaskazini utaimarika haraka.
Katika ishara nyingine ya kuonyesha kuwa Marekani
ina matumaini ya kumaliza mvutano uliopo, Kerry hakutembelea kijiji cha
makubaliano ya kusitisha mapigano cha Panmunjom, kituo ambacho kwa
kawaida viongozi wa kigeni hukitembelea, pindi wanapozuru Seoul.
No comments:
Post a Comment