Shirika la habari la taifa
la Uchina linasema kuwa watu 150 wamekufa katika tetemeko kubwa la ardhi
ambalo limeporomosha majengo na bara-bara katika jimbo la Sichuan,
kusini-magharibi mwa nchi.
Shughuli za uokozi zinatatanishwa na bara-bara zilizovunjika na simu zilizokatika.
Waziri Mkuu, Li Keqiang, aliwasili huko haraka kuongoza shughuli hizo.
Tetemeko lilotokea katika jimbo la Sichuan mwaka wa 2008 liliuwa watu 90,000.
chanzo:bbcswahili.co.uk