Search in This Blog

WALIMU HATIHATI KUFUKUZWA

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, amesema kamwe serikali yake haitosita kuwafukuza kazi  walimu wanaoshindwa kutekeleza ipasavyo majukumu yao na kusibabisha wanafunzi kufanya vibaya visiwani humo.

Alitoa onyo hilo baada ya Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) kutangaza matokeo mabaya ya kufeli kwa wanafunzi ambayo hayajawahi kutokea kwa miongo kadhaa.

Akihutubia mara baada ya kuzindua nyumba mbili za walimu katika kijiji cha Makunduchi Mzuri, mkoa wa Kusini Unguja jana, Dk Shein, aliitaka Wizara ta Elimu na Mafunzo ya Amali kusimamia majukumu yake ipasavyo, ikiwemo kuhakikisha walimu walioajiriwa ni wenye sifa na vigezo vya kitaaluma.

Alisema walimu ni lazima wafanye kazi kikamilifu ili kuinua kiwango cha elimu ambacho kimeonekana kushuka visiwani Zanzibar.

“Akibainika mwalimu anafanya kazi kinyume na sheria ni vyema kumuondoa kazini, lazima kiwango bora cha elimu kuimarishwa Zanzibar” alisema Dk. Shein.

Alisema serikali imeamua kuboresha na kuinua kiwango cha elimu Zanzibar kwa kujenga majengo ya shule za msingi na sekondari za kisasa na kutaka juhudi hizo kuungwa mkono na walimu wenyewe bila ya kushurutishwa.

“Wakati wa kubebana na kukataa muhali  umekwisha katika utendaji wa kazi, ni vyema Wizara ya Elimu ikahakikisha walimu na wakaguzi wanafanyakazi zao ili wanafunzi wajengewe uwezo na maarifa ya kufaulu katika viwango kila mwaka” alisema Rais huyo wa Zanzibar.

Dk. Sheim alisema maendeleo ya wanafunzi na lengo la serikali katika kuinua kiwango cha ubora wa elimu yatafanikiwa iwapo walimu kwa kushirtikiana na wazazi watafanyakazi kwa pamoja ya kufuatilia maendeleo ya watoto wao.

No comments:

Post a Comment

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger