Arusha: Siku saba baada ya tukio la mlipuko wa bomu katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Olasiti mkoani Arusha, Jeshi la Polisi limesema kuwa mlipuko huo ulitokana na bomu lililotengenezwa kiwandani.
Taarifa hiyo ni sehemu ya matokeo ya uchunguzi
unaofanywa kutokana na tukio hilo lililotokea Jumapili iliyopita,
kupoteza maisha ya watu watatu na kujeruhi wengine 67 baadhi wakiwa
katika hali mbaya.
Polisi nchini kwa kushirikiana na vyombo vingine
vya dola na Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) vipo katika uchunguzi
kuhusu tukio hilo lililotokea muda mfupi kabla ya kanisa hilo
kuzinduliwa rasmi ambapo mgeni rasmi alikuwa Balozi wa Vatican nchini
Askofu Mkuu Francisco Padilla.
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa
bomu hilo siyo la kutengenezwa kienyeji, bali ni la kiwandani.
“Uchunguzi wa awali unaonyesha, bomu lililotupwa
kanisani siyo la kutengeneza kienyeji. Hii ni kwa mujibu wa taarifa
tulizozipata kutoka kwa wataalamu ndani ya Jeshi la Polisi,” alisema na
kuongeza:
“Taarifa kamili itatolewa Jumatatu (kesho) kwa
kuwa kuna baadhi ya watuhumiwa wanaendelea kukamatwa na kuhojiwa na
polisi na wengine watafikishwa mahakamani.”
Kamanda Sabas alisisitiza kuwa Jeshi la Polisi
linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na halitasita kutoa taarifa kwa
umma kukiwa na haja ya kufanya hivyo, ambapo amewaomba wote wenye
taarifa zinazoweza kusaidia upelelezi kuzitoa polisi.
Arusha na Ugaidi
Taarifa hizo zimekuja huku mji wa Arusha ukianza kuingia katika rekodi mbaya ya kuhusishwa na vitendo vya ugaidi, baada ya matukio matatu kuuhusisha mji huo wa kitalii nchini.
Taarifa hizo zimekuja huku mji wa Arusha ukianza kuingia katika rekodi mbaya ya kuhusishwa na vitendo vya ugaidi, baada ya matukio matatu kuuhusisha mji huo wa kitalii nchini.
Kuhusishwa kwa mji huo na ugaidi kunatokana na
wahusika wakuu wa milipuko iliyotokea nchini na nchi jirani kudaiwa
kwamba waliratibu vitendo hivyo wakiwa katika mji huo.
Taarifa zilizopo zinaonyesha kuwa mwaka 1998
mtuhumiwa mkubwa wa ugaidi, Ahmed Khalfan Ghailani, alidaiwa kukaa kwa
muda mjini Arusha na kununua baruti za kulipulia miamba kutoka kwa
baadhi ya wachimbaji wa madini ya Tanzanite Mirerani, Wilaya ya
Simanjiro.
Baadaye ilibainika kuwa mabomu yaliyotumika
kulipua Ofisi za Ubalozi wa Marekani katika miji ya Dar es Salaam na
Nairobi nchini Kenya katika tukio la Agosti 7, mwaka huo wa 1998,
malighafi zake zilinunuliwa mkoani Arusha na Ghailani.
Katika tukio jingine la mwaka 2011, wakazi wawili
wa Arusha, Abdulmalik Majid na Hija Seleman Nyandondo (30), walikamatwa
kwa tuhuma za kushiriki njama za kuilipua kwa bomu klabu moja ya usiku
katika Jiji la Kampala nchini Uganda lililopoteza maisha ya watu 74,
waliokuwa wakitazama mpira wa Fainali za Kombe la Dunia, mwaka 2010.
Ilibainika pia kuwa bomu lililotumika lilitengenezwa Arusha kwa
kutumia baruti zinazouzwa Mirerani na baadaye kusafirishwa kwa gari
kupitia mpaka wa Namanga, Nairobi hadi Kampala.
Mbali ya matukio hayo Jumapili iliyopita mji wa
Arusha ulikumbwa na taharuki baada ya bomu kurushwa katika Kanisa
Katoliki, Parokia ya Mtakatifu Joseph, Olasiti, muda mfupi kabla ya
kanisa hilo kuzinduliwa, ambapo watu watatu walipoteza maisha na wengine
67 kujeruhiwa.
Katika tukio hilo linalohusishwa na ugaidi Balozi
wa Vatican nchini Askofu Mkuu Francisco Padilla na Askofu Mkuu wa Jimbo
Kuu Katoliki la Arusha Josephat Lebulu walinusurika, ambapo tayari watu
12 wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Msemaji wa JWTZ
Akizungumzia hali hiyo Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema kuwa uchunguzi wa mlipuko huo unavihusisha vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
Akizungumzia hali hiyo Msemaji wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Kanali Kapambala Mgawe alisema kuwa uchunguzi wa mlipuko huo unavihusisha vyombo vya ulinzi na usalama nchini.
“Bado tunachunguza na tutaeleza uchunguzi
ukikamilika kwa kuwa suala zima linachunguzwa na vyombo vya ulinzi na
usalama, ni timu kubwa inayofanya kazi hiyo,” alisema Kanali Mgawe.
Alipoulizwa uchunguzi huo utakamilika lini
alisema: “Wanaofanya uchunguzi wamejiwekea muda wao maalumu wa kumaliza
kazi hiyo, binafsi siujui, lakini ukikamilika nafikiri wataeleza
sababu.”
Udhibiti biashara ya baruti
Udhibiti hafifu wa ununuzi wa baruti katika machimbo ya madini aina ya Tanzanite eneo la Mirerani mkoani Manyara unaelezwa kuwa ndiyo chanzo cha utengenezaji mabomu kwa urahisi na kutumika na magaidi.

Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa wachimbaji
wadogo katika migodi hiyo wamekuwa wakitumia baruti hizo kutengeneza
mabomu ya kienyeji.
Uchunguzi zaidi unaonyesha kuwa wahalifu hao
wamekuwa wakikwepa kununua baruti hizo kisheria kutokana na kukosa
vibali hivyo kununua kwa njia za panya hali inayoashiria hatari ya
vitendo vya mashambulizi ya mabomu ya kutengeneza kushamiri nchini.
Baadhi ya wahalifu wamekuwa wakinunua baruti hizo
mitaani mkoani Arusha kutoka kwa wachimbaji wa wadogowadogo kutokana na
kutokuwa na vibali husika vya kununua baruti hizo.
Kauli ya Tamida
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Chama cha Wachimba Madini nchini, Sam Mollel alisema kuwa siyo rahisi kwa wachimbaji kupata kibali cha kulipua miamba katika migodi kwa kuwa kuna sheria za kupata vibali vya ununuzi wa baruti hizo na kwamba yeyote anayetaka kununua baruti lazima afuate sheria na kuomba kibali ofisi ya madini Kanda ya Kaskazini ili kununua baruti.