Search in This Blog

HILI NDIO JAMBAZI SUGU LILILOUWAWA MOROGORO....




Daktari katika hospitali ya mkoa wa morogoro akiangalia mwili wa mtu anayedaiwa kuwa ni jambazi baada ya wananchi katika kijiji cha mwanzomgumu manispaa ya morogoro kumua huku majambazi hayo nayo yakijeruhi watu wawili na kupora kiasi cha pesa sh 2.3 mil katika soko la ndizi  


kwa mujibu wa taarifa zilizotufikia zimeeleza kuwa jumla ya majambazi watatu wenye silaha yalivamia wafanyabiashara na wakulima na kufyatua risasi ambazo zimewajeruhi watu wawili na kulazwa katika hospitali ya mkoa wa morogoro.

Waliojeruhi na kutambuliwa ni furaha shomari, (30) mkazi wa mwanzo mgumu ambaye  alipigwa risasi sehemu ya ubavuni na kutokea  eneo la tumbo.endelea kupitia audifacejackson blog kwa taarifa zaidi.
mungine ni  hussein ramadhan suleiman (40) mkazi mburahani kwa jongo jijini dar es salaam ambaye naye alipigwa risasi katika ugoko wa mguu na kudondoka chini huku mmoja wa majambazi hao alimpola kiasi cha sh 2.3 mil pamoja na simu ya mkononi yenye thamani ya sh 80,000 katika tukio lililotokea majira ya saa 12 kasoro.

Baada ya kutokea tukio hilo wananchi walifanikiwa kumbidhiti mmoja wao na kumshushia kipigo hadi kupoteza maisha

 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger