Search in This Blog

KUMRADHI MSOMAJI KWA PICHA HIZI,MLINZI WA BAR ACHINJWA KAMA KUKU,NI UNYAMA WA KUTISHA

Mlinzi wa baa ya Darajani Stop Over iliyo kando kando ya barabara kuu ya Morogoro Dar es salaam jirani na daraja la Mzambarauni mkoani hapa Bw Mika Athumani  amechinjwa na majambazi usiku wa kuamkia leo.Habari zilizoptaikana eneo la tukio zilidai kwamba majambazi  hao baada ya kuvamia baa hiyo iliyojitenga usiku wa manane  na kumvamia mlinzi huyo na kumchinka kama kuku na baadae kuvunja baa hiyo na kuimba vitu mbali mbali.
  Mwili wa marehemu ukiwa ndani ya gari, la polisi kufuatia mwili huo kutenganiswa vibande viwili..

     Sehemu aliyochinjiwa mlinzi huyo aliyefahamika kwa jina Mika Athumani.
Akihojiwa na audifacejackson blog mmiliki wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi alidai kwamba majambazi hao walimvamia mlinzi wake na kumchinja na baadae walivunja Counter ya baa hiyo pamoja na duka ililipojirani na baa hiyo na kuiba vitu mbali mbali.Alipoulizwa kwamba kuna taarifa zinadai kwamba mlinzi huyo alikutwa akiwa amelala Bw Mushi alisema"endeleakupitia audifacejackson blog, inawezekana lakini hakuna mtu mwenye uhakika na jambo hilo kwani sote hatukuwepo,wakti tukio hilo linatokea"alisema Bw Mushi ambaye anadai bado hajafahami dhamani ya vitu vilivyoibikiwa na majambazi hayo.

 Mwananachi akishuhudia damu ya mlinzi huyo kwa hudhuni

 Baskeli ya Mlizni huyo ikiwa imetapakaa damu ambapo inadaiwa mlinzi huyo alikuwa amelala kwenye eneo hilo

     Redio ambayo majambazi hayo waliiangusha nje ya baa hiyo 

 Majaira ya saa 12 asubuhi ya leo wananchi walishuhudia maduka mawili ya baa hiyo yakiwa wazi huku mwili wa mlizni huyo umekutwa upande wa baa ukiwa umechinjwa na kutenganishwa kichwa na mwili

                 Umati wa watu ukishuhudia tukio hilo muda mfupi uliopita











              Gali la polisi likiondoka eneo la tukio na mwili wa marehemu



                        Wananchi nao waliondoka eneo hilo la tukio

 Mmili wa baa hiyo Bw Salvatory Mushi akihojiwa na waandishi wa habari eneo la tukio
            Majirani wa eneo hilo wakihojiwa na waandishi wa habari
                           
Baadhi ya watu waliokuwepo eneo hilo la tukio walidai kwamba mlinzi huyo alikuwa amelala hivyo majambazi hayo yalimvamia na kumpora siraha zake na kishi kumchinja shingoni," siumeona alikuwa amelala jirani na baiskeli yake ndio maana ameshindwa kupamabna nao hasa ukizingatia baa hii imejitenga iko peke yake hapa jirani na mto wa Morogoro"alisema Bw Maneo Mashani.
Mtandao huu ulishuhudia mtoto wa marehemu pamoja na mjukuu wa marehemu wakiangua vilio eneo la tuko baada ya kuuona mwili wa mazazi wao aliyeuwawa kikatili baadae wote wawili walipanda gari la polisi na kuondoka nao.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger