Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela ametumia usiku wa pili
akiwa mahututi kwenye hospitali usiku wa jana huku wanafamilia na watu
wengine duniani wakihofia kuwa shujaa huyo wa Afrika anaweza kupoteza
maisha muda wowote.
Gari chache zimeonekana leo asubuhi zikiingia kwenye hospitali hiyo ya Pretoria ambako Rais huyo wa zamani amelazwa.
Jana, Rais Jacob Zuma alisema kuwa “Rais wa zamani Mandela ameendelea kuwa mahututi hospitali.”