Siku chache kabla
ya ziara ya rais wa marekani kuja nchini tanzania imefahamika kuwa bibi yake na
rais obama mama sarah obama anatarajia kuja nchini tanzania kuja kumsalimia
mjukuu wake huyo.
Akizungumza
juzi kijijini kwake eneo la kwegero huko kisum bibi huyo aliezaliwa mwaka 1922
amesema kuwa hajiskii vibaya obama kutoitemgelea kenya kwani anajua kuwa obama
ni rais wa taifa kubwa duniani,hivyo anakuwa na ratiba ambayo inazingatia mambo
mengi na ni vigumu sana kuivunja.
Bibi huyo
ameendelea kusema kuwa anajisikia furaha kuona mjukuu wake huyo kuja tanzania
kwani historia inaonyesha kuwa kabila la kijaluo linamuingiliano mkubwa kati ya
nchi hizi mbili za tanzania na kenya hivyo wao wanaamini kuwa obama
ameitembelea nchi ya nyumbani kwao