Chuo Kikuu cha Wits cha nchini Afrika Kusini kilitayarisha tanzia ya
kifo cha rais mstaafu wa nchi hiyo, Nelson Mandela wakati bado yuko hai.
Tanzia hiyo ilitokea katika Google search kitu kilichowastua na
kuwashangaza wengi
Chuo hicho kimeomba radhi kufuatia tukio hilo na kusema tanzia hiyo imetokea Google kimakosa. Waliitayarisha ili iwe kwenye system zao za ndani lakini haikutakiwa ionekane kwa umma.
Kimesema tanzia hiyo ilitakiwa isionekane bado na iwe kwenye mitandao yao ya ndani lakini tatizo
la kiufundi limefanya ionekane kwenye Google.
Kwa kifupi ni kwamba, hawaombi radhi kwa kuandika tanzia hiyo, bali kwa tanzia hiyo kuonekana. Swali langu ni, kwanini wametayarisha tanzia wakati mzee bado yuko hai? Tanzia sio kitu kinachochukua muda mrefu kuandika kama kitabu. Sehemu kama ya Chuo Kikuu, yenye waadhishi mahiri wengi, ingewachukua chini ya lisaa limoja kuandika tanzia ya nguvu kama kifo kikitokea. Kwanini kuitayarisha kabla? Anyway, tanzia yenyewe hii hapa chini.