Search in This Blog

DIDA AELEZA ALIVYOCHUNGULIA KABURI...SOMA ALICHOKISEMA

MTANGAZAJI wa Radio Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefungua kinywa chake na kusema ugonjwa wa malaria uliompata hivi karibuni ulimfanya alichungulie kaburi kwani alihisi mauti yanamkuta.
Khadija Shaibu ‘Dida’.
Akizungumza na paparazi mapema wiki hii katika Hospitali ya Muhimbili, jijini Dar, Dida alisema kitendo cha kukutwa na malaria 250 katika mwili wake kilikuwa hatari sana kwani ingeweza kumuondoa uhai kabisa.
“Nilichungulia kaburi mwenzenu maana hali niliyokuwa naisikia siku ile ya kwanza ilikuwa ni nusu duniani, nusu akhera. Nilikuwa wa leo au wa kesho ila namshukuru Mungu kwa sasa naendelea vizuri,” alisema Dida.
Mwishoni mwa wiki iliyopita, Dida alipandwa na malaria kali, akakimbizwa katika Hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar kisha kuhamishiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa matibabu zaidi.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger