“Hii ndio siri ya RJ Comapany kuwa best production company 2013 kwenye tuzo za Steps Awards,” ameandika Ray kwenye picha ya camera hiyo aliyoiweka kwenye Instagram.
Camera hiyo imevuta attention ya muongozaji wa video za muziki nchini aliyetokea kupata umaarufu nchini kwa kutayarisha video ya Jikubali ya Ben Pol na Amani ya Moyo ya Feza Kessy, Nisher.
“Congrats to my Big Boss “Ray The Greatest” kuwa na Camera Rig Kali!! Camera ni Canon But Hiyo Rig (Nyumba) yake ni ya ukweli sana na inasaidia kurahisisha kazi iwe nzuri na ya Ki-professional zaidi. Kwenye Google inapatikana sehemu nyingi ila kwa haraka kuna jamaa wanaitwa “Redrock Micro”…check website yao…kama wewe ni director wa Video/Films/Commercials na unapenda kazi yako agiza vitu vikali,” ameandika Nisher.