Hili suala ni gumu kuliko linavyofikirika na jamii na watu ambao
hawajapatwa na mikasa migumu. Ndio maana unyanyapaa unaendelea kutawala
sana humu nchini na tatizo linazidi kushamiri. Nilikuwa na mchumba
ambaye nilimpenda sana na ndiye niliyemuweka kuwa chaguo langu la
maisha.
Mwanzoni mwa uhusiano wetu tulikuwa tukifanya mapenzi kwa kutumia condom
na baadaye tulikuja kuacha kutumia baada ya kupima several times na
kuona tupo vizuri na tulikuwa tumeshakubaliana kuja kuishi pamoja.
Nilimtambulisha kwa ndugu zangu kama ndiye ndugu yao atakayeongezeka na
yeye alinitambulisha kwa baadhi ya ndugu zake.
Miaka ilivyozidi kwenda niliona mabadiliko kwa mwenzangu kitabia kwani
kuna wakati alikuwa akinidanganya kwamba amesafiri kumbe yupo na
hajaondoka. Kumbe mwenzangu alishaanzisha uhusiano na wazee wa mujini
wenye pesa zao hivyo akawa ananipotezea kwani kwa wakati huo ndo
nilikuwa namalizia mwaka wangu wa mwisho chuoni.
Hali ilizidi kuwa mbaya zaidi kwani ilifika kipindi akanambia ile
mipango tuisitishe. nilipomuuliza kwa nini, hakuwa na jibu la wazi.
Ilinichanganya sana lakini nilipata faraja kutoka kwa rafiki zangu na
ndugu nikatulia. Baada ya miezi kama sita kupita niliamua kwenda kupima
na nikagundulika kwamba niko na maambukizi ya VVU, nilichanganyikiwa
sana na niliona kama hakuna haja ya kuishi tena.
Sikumwambia mtu mwingine zaidi ya doctor mmoja na mimi mwenyewe kuugulia
maumivu yangu peke yangu ila kuna wakati ndugu na jamaa walikuwa
wakiniona nimebadirika ila nawaambia hakuna shida yoyote na nipo
kawaida. Nilijitahidi kutokukaa peke yangu kwani mawazo ndo
yangenizidia.
Mpaka sasa hivi nipo vizuri na nna afya njema ila napata wakati mgumu
sana kwani wasichana wengi wanaonesha dalili za kutaka kuwa na uhusiano
na mimi lakini nawaonea huruma sana kwani inaniuma sana nikifikiria
kumwambukiza mtu mwingine. Wengi wao nimekuwa nikiwakwepa mpaka wengine
wananitangazia kwamba jogoo wangu hawiki, huwa inaniuma sana kwani
sitaki wajue na sipendi kuwafanya wawe kama mimi.
Nisiwasumbue sana, naomba nihitimishe kwa kusema; hili tatizo ni gumu
sana hasa unapokuwa wewe ndiwe 100%. Tupigeni vita unyanyapaa ili watu
wasiwe na mawazo ya kwamba TUFE WENGI. Pia unayemnyanyapaa hujui
aliupata vipi kwani si kila mwenye VVU alikuwa kuruka njia. Kuna wengine
wameupata kutoka kwa watu wanaowaamini sana! Na wengine miaka ya leo
wamezaliwa nao hivyo sio kosa lao kwa hapo walipo.