Rachel Haule ‘Recho’.
MWIGIZAJI
wa sinema za Kibongo, Rachel Haule ‘Recho’ alijikuta akichezea kibao
cha ukweli na kusababisha aangue kilio wakati alipokuwa akirekodi
sinema. Akizungumza na Stori 3, sosi aliyeshuhudia tukio hilo
lililotokea maeneo ya Mwenge, jijini Dar alisema msanii huyo alikuwa
katika kurekodi moja ya vipande vya sinema yake mpya lakini kutokana na
matakwa ya filamu hiyo kuonesha hisia za kulia, ilibidi Baba Haji
amshushie kofi fastafasta.
“Siku hiyo sikuwa kwenye ‘mudi’ sababu kuna mambo yalinichanganya, nilishindwa kuvuta hisia za kulia ndipo niliposhtukia kofi la Baba Haji na machozi yalinitoka yenyewe, hii kazi yetu hii we acha tu,” alisema Recho.