Msanii wa muziki wa kizazi kipya nchini Kenya Ibra Da Hustler akiwa katika pozi
WAKATI
kesho dunia inaadhimisha siku ya matuizi ya dawa za kulevya Rapper Ibra
Da Hustler amefunguka kuwa sasa anampango wa kubadilisha maisha yake
kwa uamuzi aliouchukuwa wa kuachana na matumizi ya dawa aina ya Herion
na Crack Cocaine.
Da Hustler ameamua kuachana na matumizi hayo ya
dawa za kulevya baada ya kuona kuwa ni uharibifu wa pesa pili kitendo
hicho ni kukaribisha dharau kwenye maisha yake huku akihatarisha maisha,
Rapper huyo ambaye kwa sasa ana takribani siku nne hajagusa toka
amejiunga na taasisi amejifunza kuvumilia na matumaini yake ni kuachana
kabisa na matumizi hayo ya dawa za kulevya.
Akizungumza nachanzo cha habari, alisema kwamba mwanamke ndiye aliyemshawishi mpaka
akiingiza katika matumizi ya dawa ya kulevya. “Kuna binti alinishawis
kutumia dawa na ndio nikajikuta nimeingia katika mkumbo huu najuta
kumfahamu nakubaini kuwa hataki maendeleo yangu kabisa nanimejifunza
kutoka kwake, sasa nikimwambia mtu usiguse dawa ataamini kwani najua
kitu gani atapata kwenye maisha yake”alisema Dar Hustler.
“Nimeacha
Kabisa madawa nina siku nne sijagusa toka nimejiunga na hii taasisi ya
kuwaelimisha watu wanaohitaji kuachana na dawa za kulevya, nimejifunza
kuvumilia arosto na matumaini yangu ni kuacha kabisa dawa kwani
yameharibu maisha yangu kabisa".
Alisema kwamba matumizi ya dawa za kulevya ni uharibifu wa pesa nyingi na kwamba amekaribisha dharau kwenye maisha yake.
Rapper
huyo alisema endapo atafanikiwa kuachana na matumizi ya dawa za kulevya
atarudi katika kazi yake ya muziki, kwani anaamini ndiyo kazi pekee
anayoiweza na mashabiki wake watakuwa wamemis kazi zake."Kundi la
wanamuziki wa Nako 2 Nako na Weusi wananipa ushirikiano mzuri sana, wote
wamefurahi kusikia nimeanza kuachana na dawa za kulevya".
akizungumzia
wimbo wake wa sababu ni wewe, anasema kwamba,"niliimba mambo yote
yaliyonitokea tangu nilipoanza kutumia dawa ya kulevya na jinsi yalivyo
niharibia maisha yangu, matumaini yangu kwa vijana wanaotumia dawa
watajifunza kutoka kwangu kuhusu madhara ya dawa za kulevya.