Search in This Blog

PADRI ASHINIKIZA MAPADRI KANISA KATOLIKI WARUHUSIWE KUTOA MAPEPO

KUSHOTO: Padri Gabriele Amorth. KULIA: Papa Francis I akimtoa mapepo mmoja wa walemavu.

Mpungaji mapepo' anayeongoza katika Kanisa Katoliki ametaka mapadri wote kuruhusiwa kuendesha misa za tambiko baada ya Papa Francis kufanya moja hadharani St Peter's Square hivi karibuni.
Padri Gabriele Amorth, mkuu wa Shirikisho la Kimataifa la Wapungaji Mapepo, anataka sheria za sasa zinazotaka mapadri wote kuomba kibali cha kupunga mapepo kwa maaskofu wao kulegezwa.
Padri Amorth, ambaye anadai ameshapunga mapepo 160,000, alisema ombi lake limechochewa na Papa Francis kufanya kile ambacho anasisitiza kuwa ni upungaji mapepo kwa mtu mmoja wa Mexico aliyekuwa 'akimilikiwa na mashetani wanne'.
Alieleza: "Atamwomba Papa kuwapa mapadri wote nguvu ya kutoa mapepo, na kuhakikisha mapadri wanapatiwa mafunzo sahihi katika hilo kuanzia kwenye seminari.
Kuna mahitaji makubwa kwa ajili yao."
Maoni yake yamekuja baada ya Papa Francis kunaswa kwenye filamu akifanya utoaji mapepo hadharani Mei 19.
Picha hizo zimeonesha Papa Francis akiweka mikono yake kichwani mwa mlemavu ambaye anaonesha kupata wazimu wa misukosuko na kutetemeka, kabla ya kujibwaga huku Papa akimwombea.
Padri Amorth, mwenye miaka 88, alieleza "Papa huyo pia ni Askofu wa Roma, na kama ilivyo kwa askofu yeyote yeye pia ni mpungaji mapepo."
Wote ambao wanaochukulia upungaji mapepo kama ushirikina walikuwa wanakosea akisisitiza: "Kwa sasa kuna, zaidi kuliko ilivyowahi kutokea, mahitaji ya upungaji mapepo kupambana na watu wanaoshikiliwa na 'mizimu' na 'mashetani'."
Baba Mtakatifu huyo alitambulishwa kwa wanaume wawili waliokuwa kwenye viti vya magurudumu baada ya Ibada ya Pentekoste iliyofanyika Jumapili.
Wakati padri mmoja alipochomoza na kumweleza kitu fulani Papa Francis, Papa huyo alionekana kuchukulia kwa uzito wa kipekee.
Kisha Papa akamshika kichwani mtu huyo kwa makini, akamwinamisha chini kwenye kiti chake. Huku akimwombea sala maalumu, mdomo wa mtu huyo ukaachama wazi na kupumua kwa nguvu zaidi ya mara sita, akionekana dhahiri kutikisika.
Baada ya tambiko hilo Francis aliendelea na mikutano yake ya kawaida na wagonjwa ambao walifika kanisani hapo.
Uongozi wa Vatican umetolea ufafanuzi tukio hilo huku msemaji Padri Federico Lombardi alisema Papa huyo 'hakukusudia kufanya utoaji mapepo' ila 'maombi kwa mtu mwenye maradhi'.
Lakini Padri Amorth anasisitiza 'maombi' hayo yalikuwa tambiko la utoaji mapepo. Alieleza: "Padri yule alimweleza Papa: "Tazama, huyu ni kijana anayemilikiwa na mashetani wanne". Na Papa huyo alimbariki na kumwombea, hakika ilikuwa na dhahiri upungaji mapepo.
"Upungaji mapepo huo wa papa ni ishara nzuri sababu moja ya chanzo kikuu cha ukanaji Mungu wa sasa ni kwamba watu hawaamini tena katika Shetani. Yesu alisema: "Yeyote ambaye hayuko nami yuko na Shetani"."
Aliongeza: "Tunaishi katika zama ambazo Mungu amesahaulika. Na kote huko Mungu hayuko, Shetani anatawala.
"Leo, kwa bahati mbaya, maaskofu hawaruhusu upungaji mapepo wa kutosha. Tunahitaji mwingi zaidi. Natumaini kwamba Roma itatoa maelekezo kwa maaskofu kote duniani kuwataka kutoa ruhusa za wapungaji mapepo zaidi."
Papa wa zamani, Benedict XVI, hakuwahi kufanya upungaji mapepo rasmi lakini John Paul II anafahamika kuwahi kufanya upungaji mapepo takribani mara tatu katika kipindi chake.
Padri Amorth alidai Papa John Paul II amekuwa mpungaji mapepo mwenye nguvu mno. Alisema: "John Paul II alipambana mara nyingi zaidi dhidi ya Shetani.
"Japo amefariki, bado yupo leo katika upungaji mwingi wa mapepo. Kama utataja jina lake wakati wa upungaji mapepo, mtu ambaye anashikiliwa na mashetani hutokwa na mapovu mdomoni."
Padri Amorth, ambaye ameshikilia nafasi hiyo kwa miaka 28, anafahamika kwa tabia yake ya kuropoka na siku za nyuma aliwahi kushutumu yoga na Harry Potter.
Alisema: "Kufanya yoga kunaleta ushetani kama ilivyo kumsoma Harry Potter. Vyote vinaweza kuonekana kawaida lakini vyote vinahusika na mazingaombwe na hivyo vinaelekeza kwenye ushetani."
Mwaka 2006, Padri Amorth, ambaye alipata daraja hilo mwaka 1954, alifanya mahojiano na Radio Vatican ambako alisema kwamba kiongozi wa Nazi Adolf Hitlet na dikteta wa Urusi Josef Stalin wote walikuwa wakimilikiwa na Shetani.
 
Support : KARIBU TENA MDADISI MAM
Copyright © 2011. RISASI - Haki Zote Zimehifadhiwa.
KWA HISANI YA MDADISI MAMBO
Proudly powered by Blogger